“Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Nyusi na Mwenyekiti wa SADC, huyu ndiye ‘Boss’ wetu wa SADC wa sasa kwa nchi zote 16″- Rais Magufuli akizungumza mara baada ya Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato, Geita, hii leo Januari 11, 2021.
–
Rafiki yangu nakushukuru sana kwa kuja Chato, Rais wa Msumbiji anafahamu Kiswahili, anayajua maisha ya Watanzania, urafiki kati ya hizi nchi mbili ni wa muda mrefu, sisi ni ndugu na ndani ya serikali tuna makubaliano ya kufanya kazi pamoja”- Rais Magufuli.
–
“Rais Nyusi alinipigia simu akaniambia nataka kuja Chato, alisikia mimi nipo Chato, akasema nataka tuje tuzungumze masuala ya maendeleo, nawashukuru sana Wizara Afya kwa kuona hospitali hii iwekwe jiwe na Rais wa Msumbiji”- Rais Magufuli.
NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu
Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Nkwingwa...
Read more