Wanajeshi wa Ghana jana walilazimika kuingilia kati kizaazaa kilichozuka bungeni ambapo vyama viwili vikubwa vilipambana na kusababisha vurugu karibu usiku mzima katika zoezi la kuapisha wabubnge.
Ghasia hizo ziliibuka baada ya mbunge wa chama tawala kujaribu kuling’ang’ania sanduku la kura wakati wakipiga kura za kumchagua spika.
Ugomvi huo ulidumu kwa saa kadhaa hadi jeshi lilipoingia bungeni huku kasheshe lote hilo likionekana live kwenye televisheni.
“Kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa sheria na kanuni,” alisema mbunge mteule Kwame Twumasi Ampofo wa chama cha upinzani National Democratic Congress (NDC).