Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mhe.Maalim Seif amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuendeleza na Kuimarisha umoja na mshikamano katika visiwa vya Pemba na Unguja, leo ikulu Ndogo Chato.
“Niseme tulikua na mazungumzo mazuri mazungumzo ya kidugu na mazungumzo ambayo mimi natumaini kwamba Kiongozi wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yuko pamoja na sisi, hasa katika swala zima la kuimarisha umoja, Upendo na Maelewano katika visiwa vya Unguja na Pemba.
“Nimefarijika sana kumsikia mwenyewe Mheshimiwa Rais akituhakikishia kwamba yuko pamoja na sisi na atatuunga Mkono kwa hali na Mali kwahivyo Mheshimiwa Rais nakushukuru sana,”.