Maisha Magic Bongo chaneli namba 160 kupitia king’amuzi cha DStv imewazidishia uhondo wa burudani watazamaji wake baada ya kuja na tamthilia mpya zitakazokonga mioyo ya wapenzi wa tamthilia kutokana na ubora wa tamthilia hizo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthilia mpya ya Jua Kali na Pazia zitakazoanza kurushwa kuanzia januari 2021 kwenye chaneli ya MMB Dstv 160, katibu mtendaji wa bodi ya filamu Tanzania Dr. Kiagho Kilonzo, amesema kuwa serikali inathamini na kutambua mchango mkubwa wa MultChoice katika kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu hapa nchini. amesema kitendo cha chaneli ya Maisha Magic Bongo kuwa na maudhui mengi ya ndani kimekuwa kumekuwa ni chachu ya ajira nyingi katika tasnia lakini pia kumeongeza ushindani na ubora wa kazi za uzarishaji wetu.
Pia ameongeza kuwa yeye binafsi amekuwa akiwatembelea wasanii na kujionea uzarishaji wa filamu na maudhui mengine.
Kilonzo amewataka wasanii kutumia fursa hii vizuri na kuhakikisha kuwa wanaongeza ubora wa kazi zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje na hivyo tasnia ya filamu kuongeza mchango wake katika uchumi wa wasanii na taifa kwa ujumla.
Naye mkuu wa masoko wa MultChoice Tanzania Ronald Shelukindo, amesema mbali na kutumia wasanii na waigizaji wakongwe , wamehakikisha kuwa kuna mchanganyiko na waigizaji wapya na vijana ambao wanaleta vionjo vipya na vya kisasa na kuzifanya tamtilia hizo kuvutiwa na watazamaji wa rika zote.
“kila mara tunaleta maudhui kulingana na matakwa ya wateja wetu, tunahakikisha kuwa tunawapatia maudhui yetu.”
Pia Ronald ameongeza kuwa wanafurahi sana kufanya kazi na wazalishaji wa waigizaji Tanzania na hivyo kuzid kukuza vipaji vya wasanii wetu na kuwapa ulingo wa kuonyesha umahiri wao katika fani.
Tamthilia mpya ya Pazia inaonekana kuanzia Jumatatu hadi jumatano saa 1:30 jioni. Huku tamthilia ya ya jua kali itaanza kutingisha jiji leo januari 6,2021 kuanzia saa 3:30 usiku jumatano hadi ijumaa.