Nyota wa Manchester United Paul Pogba alisema Mashetani Wekundu wako tayari kwa pambano lao dhidi ya Liverpool baada ya kuwa kileleni mwa Ligi ya Premia.
United ana alama tatu mbele ya wapinzani wao Liverpool kabla ya pambano la Jumapili huko Anfield.
“Utakuwa mchezo mzuri kwa kila pande,” Pogba aliiambia BBC Sport,
“Ni mchezo mkubwa unaokuja kwa hivyo tujiandae.”
United, wakati huo huo, hawajafungwa katika mechi zao 15 za ugenini kwenye Ligi ya Premia tangu waliposhindwa 2-0 na Liverpool mnamo Januari mwaka jana, vilevile Liverpool hawajawahi fungwa uwanja wa nyumbani.
“Tulijua ikiwa tutashinda usiku wa leo tutakuwa juu ya ligi tutakapocheza na Liverpool,” alisema Pogba,
“Tunapaswa kutulia, sasa ni wakati mzuri. Tutaona nini kitatokea.”