Mvua zinazoendele Mtwara zimesababisha watu kukosa makazi ikiwa ni nyumba 177 zikisombwa na maji huku nyumba 315 zikijaa maji kutokana na mvua kali zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo.
Serikali iliandaa kambi mbalimbali kuwahifadhi waathirika wa janga hilo ambapo ilitenga Shule na Vyuo lakini Mkuu wa Mkoa, Gelasius Byakanwa, amesema watu walioharibiwa makazi walilala kwa jamaa zao.
Byakanwa amesema hali si nzuri ambapo amewashauri Wananchi wafike maeneo yaliyopangwa ili kusaidiwa kwa urahisi zaidi hasa huduma za kibinadamu
Taarifa kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa inaonesha Mvua zitaendelea Kunyesha hivyo, Wananchi wanatakiwa kutoka katika maeneo yenye maji na kwenda sehemu zilizotengwa kwaajili ya usalama wa maisha yao.