Naibu Waziri Kipanga asimamisha kazi maafisa wanne VETA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Naibu Waziri Kipanga asimamisha kazi maafisa wanne VETA

Mhariri by Mhariri
Jan 11, 2021
in HABARI
0 0
0
Naibu Waziri Kipanga asimamisha kazi maafisa wanne VETA
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia mhe. Omary Kipanga amewasimamisha kazi maafisa wanne wa chuo cha ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Mkoa wa Lindi.

Mhe. Kipanga amefikia maamuzi hayo wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA cha wilaya ya Mafia ambacho ujenzi wake unasimamiwa na chuo cha VETA Lindi.

Mhe. Kipanga amesema amechukua hatua hiyo baada ya kugundua ukiukwaji mkubwa wa taratibu katika kutunuku zabuni ikiwemo kumtunuku mwalimu wa chuo cha VETA Lindi aliyefahamika kwa jina la Rose Mlelwa na mafundi kufanya kazi bila ya mikataba.

Watumishi hao wa chuo cha VETA Lindi waliosimamishwa ni Mkuu wa chuo, Afisa Ugavi na manunuzi, Mhasibu na Mkaguzi wa ndani ambapo mhe. Kipanga ameagiza ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mafia na Lindi kuwachunguza iwapo hawakuwa na maslahi binafsi katika kusimamia ujenzi wa mradi huo.

“Kuanzia leo nawasimamisha kazi Mkuu wa VETA Lindi, Afisa manunuzi, Mhasibu na Mkaguzi wa ndani ili kupisha uchunguzi na nawaagiza Takukuru Mafia mshirikiane na Lindi kuwachunguza hawa ili tujue kama hawakuwa na maslahi binafsi kwenye mradi huu,” amesema Naibu Waziri Kipanga.

Aidha, Naibu Waziri Kipanga amewasimamisha mafundi wote waliopewa kazi ya ujenzi wa majengo zaidi ya moja na kuwataka kila mmoja ajenge jengo moja tu kama utaratibu unavyotaka, kutokana na mafundi hao kutokuwa na nguvukazi ya kutosha kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa na amewataka wanaosimamia mradi kuhakikisha wanapatikana mafundi wengine haraka ili kukamilisha ujenzi huo.

ADVERTISEMENT

“Nataka mafundi wote waliopewa kazi ya kujenga zaidi ya jengo moja wabakie na ujenzi wa jengo moja tu sababu hawana uwezo wa kutosha kukamilisha ujenzi kwa wakati na hivyo watasababisha ujenzi kuzidi kuchelewa,” amesisitiza mhe Kipanga.

Awali, akisoma taarifa ya ujenzi kwa niaba ya Mkuu wa chuo cha VETA Lindi, Richard Shekidele amesema kuwa mpaka sasa kiasi cha Sh. Bilioni 1.1 kimeshapokelewa kwa ajili ya mradi huo na kwamba ujenzi umefikia asilimia 31.5.

Serikali inajenga jumla ya vyuo ya VETA 25 katika Wilaya mbalimbali nchini vitakavyogharimu Sh. Bilioni 1.6 kila kimoja.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma
HABARI

Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma

by Mhariri
Jan 15, 2021
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano...

Read more
NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

Jan 15, 2021
Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Jan 15, 2021
Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Jan 15, 2021
Serikali yawakaribisha wawekezaji katika sekta ya mawasiliano hapa nchini

Serikali yawakaribisha wawekezaji katika sekta ya mawasiliano hapa nchini

Jan 15, 2021
Waziri Aweso asitisha agizo la EWURA kupandisha Ankara za Maji

Waziri Aweso asitisha agizo la EWURA kupandisha Ankara za Maji

Jan 15, 2021
Next Post
Mgonjwa wa kwanza kupandikizwa moyo bandia atoka Hospitali

Mgonjwa wa kwanza kupandikizwa moyo bandia atoka Hospitali

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In