Njombe TC wakabidhi taulo za kike kwa wanafunzi, DC atoa neno – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Njombe TC wakabidhi taulo za kike kwa wanafunzi, DC atoa neno

Mhariri by Mhariri
Jan 7, 2021
in HABARI
0 0
0
Njombe TC wakabidhi taulo za kike kwa wanafunzi, DC atoa neno
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Amiri Kilagalila-Njombe

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameonya na kuwatahadharisha wasimamizi wa wanafunzi watakaothubutu kuchepusha na kuingiza sokoni taulo za kike zilizokabidhiwa kwa shule 24 za sekondari mjini Njombe kwa ajili ya matumizi ya wasichana waliopevuka wanapokuwa hedhi.

Ruth Msafiri ametoa onyo wakati akikabidhi vifaa hivyo vlivyonunuliwa na halmashauri ya mji wa Njombe kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kuongeza muda wa kuhudhuria vipindi darasani pamoja na kuongeza ufanisi katika elimu kwa wasichana.

“Sio mtoto anapewa taulo siku mbili harafu hazionekani tena.Na kuna wengine wakipewa hizi zinaingia kwenye biashara,hilo ni kosa kubwa”alisema Ruth Msafiri

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminatha Mwenda,amesema wamefanikiwa kununua vifaa hivyo boksi 260 za taulo za kike zenye thamani ya zaidi ya milioni 9 kupitia mapato yao ya ndani na kukabidhi shule 24 kwa ajili ya wasichana 5636 waliopevuka ili kuwasitiri wanapokuwa hedhi.

ADVERTISEMENT

“Tumenunua taulo za kike kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa wasichana ya kusoma vizuri,na katika bajeti yetu tumetenge Milioni 10 kwa ajili ya sekondari,na Milioni 10 kwa ajili ya shule za msingi.Leo tumewakabidhi sekondari”alisema Iluminatha Mwenda

Valeno Kitalika ni mkuu wa shule ya sekondari Joseph Mbeyela,kwa niaba ya wakuu wa shule wameishukuru serikali kwa msaada huo kwa ajili ya watoto kwa kuwa wataongeza ari ya kujisomea huku akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitolea.

“Nimshukuru mkurugenzi na serikali ambao wameweza kutoa vifaa hivi kwa watoto,hawa watoto sasa wataongeza ari ya kusoma kwasababu ni vitu ambavyo vilikuwa vinawakwamisha kutokana na mahudhurio kuwa hafifu”alisema Valeno Kitalika

Elizabeth Mbigile ni mwanafunzi kutoka shule ya sekondari ya wasichana Josephine na Steria Muta ni kutoka shule ya Sekondari  Maheve.Wameshukuru serikali kwa msaada huo huku wakiendelea kuwasaidi kwa kuwa shule zingine ziko mbali na maeneo ya huduma.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais
HABARI

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais

by Ombeni Osward
Jan 16, 2021
0

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania...

Read more
Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Jan 16, 2021
Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Jan 16, 2021
Mseveni ashinda Urais tena

Mseveni ashinda Urais tena

Jan 16, 2021
Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Jan 16, 2021
Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Jan 16, 2021
Next Post
RC Kunenge aja na mkakati wa kudhibiti tatizo la uchafu wa mazingira

RC Kunenge aja na mkakati wa kudhibiti tatizo la uchafu wa mazingira

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In