Njombe: Wabunge waandaliwa nondo kushauri serikali kufuta leseni mfu za madini  – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Njombe: Wabunge waandaliwa nondo kushauri serikali kufuta leseni mfu za madini 

Mhariri by Mhariri
Jan 11, 2021
in HABARI
0 0
0
Njombe: Wabunge waandaliwa nondo kushauri serikali kufuta leseni mfu za madini 
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Njombe wamesema wapo tayari kuandaa ripoti zinazohusu leseni za vitalu vya madini visivyofanya kazi mkoani humo na kuwakabidhi wabunge ili kuwasilisha katika bunge kuona uwezekano wa kufuta umiliki wa vitalu hivyo.

Kupitia kikao cha ushauri mkoa wa Njombe (RCC) wakati wa kuchangia hoja,mkurugenzi wa halmasahauri ya wilaya ya Njombe Juma Ally amesema wapo tayari kuandaa taarifa za kutosha na kuwakabidhi wabunge ili kufikisha bungeni kwa ajili ya kuwafutia leseni wamiliki wote waliohodhi vitalu na kushindwa kufanya kazi.

Awali kaimu afisa madini mkoa wa Njombe Fredrick Gurenga wakati akisoma taarifa ya utekelezaji katika sekta ya madini alisema mkoa wa Njombe unaleseni nyingi za uchimbaji wa madini lakini hazifani kazi.

“Mfano Ludewa tuna leseni 201za uchimbaji mdogo lakini zinazofanya kazi ni 3 tu,ukija Makete kuna leseni 34 lakini zinazofanya kazi ni 4,Wangimg’ombe zipo leseni 20,na zinzofanya kazi ni 10 hususani kwenye mchanga,hapa Njombe zipo leseni 7 alikini zinazofanya kazi ni 6 walau”alisema Fredrick Gurenga

ADVERTISEMENT

Aliongeza “Kwa ujumla tuna leseni 312 lakini zinazofanya kazi ni 30,ukija kwenye uchimbaji wa kati kama za kwenye liganga na mchuchuma tuna leseni 4 na hizi zote hazifanyi kazi,kwenye leseni za utafiti ni changamoto kuwa zaidi kwasababu kuna leseni 68 na hakuna inayofanya kazi.Sisi tumeandika barua kwa wizara ya madini na tumependekeza maeneo yafutwe ili wapatikane wachimbaji wanaoweza kufanya kazi”alisema tena Gurenga

Naye mbunge wa Jimbo la ludewa Njombe wakili Joseph Kamonga,ameishauri serikali kufuta leseni za wamiliki wa vitalu vya madini wilayani Ludewa ambao hawafanyii kazi maeneo hayo ili kutoa nafasi na fursa kwa wachimbaji wadogo wenye uwezo  wa kuyaendeleza.

“Tumeshashuhudia kwenye Tanzanite tunapata Bilionea ambao wako jirani na mradi husika,pendekezo langu ni kwamba hizi leseni 201 zifutwe bila kumuonea aibu mtu yeyote,halafu watu wa madini wafike kwa wachimbaji wadogo wanaogundua madini kutokana na  kufukua fukua  ili wawaelimishe namna ya kupata haki ya kumiliki vitalu ” Alisema Kamonga.

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amesema hoja hizo ni za msingi huku akiahidi kutoa ushirikiano kwenye uwezekano kwa wabunge hao ili kufikisha hoja na bungeni na kutetea maeneo yaliyoshikiliwa kwa muda mrefu bila kutumika.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu
HABARI

NMB yatoa msaada wa mabati kutekeleza agizo la Waziri Mkuu

by I am Krantz
Jan 15, 2021
0

 Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Nkwingwa...

Read more
RC Mahenge aliagiza Jiji la Dodoma kudhibiti Ujenzi Holela wa makazi

RC Mahenge aliagiza Jiji la Dodoma kudhibiti Ujenzi Holela wa makazi

Jan 15, 2021
Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma

Picha: Makamu wa Rais aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Chamwino Dodoma

Jan 15, 2021
NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne, zijue shule 10 zilizoongoza

Jan 15, 2021
Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Kisa cha kweli: Mapenzi ya Chuo yawachanganya, waenda kanisani kula kiapo

Jan 15, 2021
Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Rais wa Uturuki apewa chanjo ya Corona

Jan 15, 2021
Next Post
Baada ya kuvunja na pora, wezi wajisalimisha wenyewe kwa kwenye duka, fahamu kilichowapata

Baada ya kuvunja na pora, wezi wajisalimisha wenyewe kwa kwenye duka, fahamu kilichowapata

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In