Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali ina mkakati wa kuhakikisha kumbukumbu zote muhimu za Nchi zinatolewa kwa Kiswahili na kuhimiza haja ya kuwepo Sera ya Kiswahili.
Mhe. Samia aliyasema hayo alipokuwa akifungua Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Jijini Dodoma ambapo amezitaka Wizara za Habari Tanzania Bara na Visiwani zikae na Wataalamu kubaini Maeneo na Nyaraka za Kiserikali ambako bado Kiswahili hakitumiki.