Akaunti rasmi ya Rais wa Marekani Donald Trump imeruhusiwa kutuma ujumbe katika mtandao wa twitter baada ya kufungiwa kwa takribani saa 12.
Baada ya kufunguliwa akaunti hiyo Bw. Trump alichapisha ujumbe wenye maudhui ya maridhiano, baada ya kufungiwa kwa kuchapisha madai ya uwongo kuhusu wizi wa kura.
Aidha Twitter ilisema kwamba itampiga marufuku kabisa rais Trump iwapo atakiuka sheria za mtandao huo wa kijamii kwa mara nyengine.