Washindi 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata – Mwanaharakati Mzalendo
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Washindi 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata

I am Krantz by I am Krantz
Jan 27, 2021
in HABARI
0 0
0
Washindi 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata
0
SHARES
24
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Meneja Idara ya Kadi wa Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa (kati kati ), akimkabidhi mshindi wa promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida – Rose Marealle mkazi wa Mbezi Inn– jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka mshindi kwenye shindano la promosheni hiyo. Rose amejishindia friji, rice cooker, water dispenser pamoja na microwave. Akishuhudia ni Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mbezi Louis, Nestory Mwombeki.

 


Mwanahabari, Masoud Kipanya ambaye pia ni Balozi wa Benki ya NMB  akizungumza na mmoja wa washindi wa Droo ya mwezi wa pili ya  Promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida  iliyochezeshwa Makao Makuu ya NMB-  jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir na kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Upendo Albert.


Mwanahabari, Masoud Kipanya ambaye pia ni Balozi wa Benki ya NMB  akizungumza na mmoja wa washindi wa Droo ya mwezi wa pili ya  Promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida  iliyochezeshwa Makao Makuu ya NMB-  jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Biashara ya Kadi wa Benki ya NMB, Philbert Casmir na kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Upendo Albert.

 Washindi 12 wa droo ya mwezi wa pili ya NMB Mastabata Siyo Kikawaida, wamepatikana leo na kujizolea zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 28.8, hivyo kufanya zawadi zilizotolewa kufikia thamani TZS 87.6 kati ya zaidi ya Sh. Mil. 200 zinazoshindaniwa.

 Promosheni ya Mastabata Siyo Kikawaida inayoendeshwa na Benki ya NMB, ni kampeni inayolenga kuhamasisha matumizi na manunuzi kwa Kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR, ilianza Novemba 24, 2020, ikitoa zawadi za Sh. 100,000 kwa washindi 40 kila wiki na washindi 12 wa Sh. Mil. 2.4 kila mwezi kila mmoja.

 Akizungumza wakati wa droo hiyo ambayo ni ya pili kati ya tatu za mwezi, Mkuu wa Biashara ya Kadi wa NMB, Philbert Casmir, amesema katika droo saba zilizotangulia (sita za wiki na mbili za mwezi), zimewawezesha washindi wapatao 304 kujizolea zawadi za TZS. 87.6

 Casmir amebainisha kuwa, NMB Mastabata imebakisha droo 3 kukamilisha miezi mitatu ya kampeni hiyo, ambayo zawadi kuu ‘Grand Finale’ itakuwa ni ziara ya utalii Zanzibar, Ngorongoro ama Serengeti, iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB, ambako washindi watakuwa huru kuchagua zawadi mbadala.

 “Wito wetu kwa wateja wa NMB kuendelea kufanya matumizi na manunuzi mbalimbali kwa Kadi za NMB Mastercard na Mastercard QR, ili kujiongezea nafasi sio tu ya kushinda zawadi za wiki na mwezi, bali ziara hii ya kitalii katika moja kati ya maeneo hayo matatu,” amesema Casmir.

 Katika droo ya leo, iliyofanyika chini ya usimamizi wa Ofisa kutoka Bodi ya Michezo Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Albert, washindi 12 walikuwa huru kuchagua zawadi zilizogawanywa katika makundi matatu, kila moja likiwa na zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 2.4.

 Katika kundi la kwanza kulikuwa na zawadi ya simu ya Samsung Galaxy Note20 yenye thamani ya Sh. Mil. 2.4, kundi la pili friji, water dispenser, Microwave na Samsung A21 kwa pamoja. Kundi la tatu ni runinga (flat screen inchi 40) iliyolipiwa DSTV miezi mitatu, laptop na simu aina ya Samsung A21.

I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe
HABARI

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe

by I am Krantz
Feb 26, 2021
0

Nilizaliwa katika familia masikini sana na wakati...

Read more
Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Feb 26, 2021
Auto Draft

FAINALI NMB MASTABATA WIKI IJAYO, 424 WAZOA ZAWADI

Feb 24, 2021
Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Feb 23, 2021
BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

Feb 23, 2021
Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Feb 23, 2021
Next Post
Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi wa JazaTukujaze Tena

Tigo yakabidhi zawadi kwa washindi wa JazaTukujaze Tena

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec   Feb »
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In