Waziri Mkuu amezindua barabara ya Matemwe hadi Muyuni – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Waziri Mkuu amezindua barabara ya Matemwe hadi Muyuni

Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mhariri by Mhariri
Jan 8, 2021
in HABARI
0 0
0
Waziri Mkuu amezindua barabara ya Matemwe hadi Muyuni
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua barabara ya Matemwe hadi Muyuni yenye urefu wa kilomita 7.58 iliyojengwa na Kampuni ya China Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) kutoka China kwa gharama ya shilingi bilioni 5.48 zikiwa ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

“Barabara hii ni kiungo muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na maeneo mengine ya mashariki mwa Kisiwa cha Unguja kwani imeungana na barabara nyingine kuanzia maeneo ya Chwaka kuelekea Uroa, Pongwe, Kiwengwa, Pwani Mchangani, Matemwe hadi Muyuni.

Waziri Mkuu amezindua barabara hiyo jana (Alhamisi, Januari 7, 2021) akiwa katika Wilaya ya Kaskazini A, mkoa wa Kaskazini Unguja, kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya kutimiza Miaka 57 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Amesema uzinduzi huo ni kielelezo cha juhudi kubwa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha miundombinu ya barabara Mijini na Vijijini kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wote wa Zanzibar.

“Hii itakuwa ni chachu kubwa ya kurahisisha shughuli za kiutalii na sekta nyingine zikiwemo kilimo, uvuvi na biashara kuelekea katika kujenga na kuimarisha uchumi wetu. Kwa msingi huo, nitoe wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zinazojitokeza kutokana na uwepo wa barabara hii ili kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na uchumi wa Zanzibar kwa ujumla.”

ADVERTISEMENT

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema uwepo wa barabara hiyo utawarahisishia wakaazi na wageni katika maeneo ya Matemwe, Mbuyu Tende hadi Muyuni na maeneo mengine ya Mkoa wa kaskazini kuondokana na adha ya usafiri waliyokuwa wakikabiliana nayo kabla ya ujenzi wake.

Waziri Mkuu amesema ni vyema wananchi wote wakatambua kwamba kupatikana kwa mafanikio hayo katika sekta ya barabara kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwepo kwa umoja na mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ili kuharakisha maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kuwa inawawezesha wananchi wake katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii kwa kuwapatia huduma bora za msingi katika maendeleo ikiwemo kuendelea kuzijenga barabara mbalimbali Mijini na Vijijini, Unguja na Pemba.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wote wa Zanzibar kuepuka kujenga ndani ya eneo la hifadhi ya barabara (road reserve) kwa lengo la kuondoa usumbufu wakati wa upanuzi wa barabara na miradi mingine ya maendeleo.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa namna alivyoanza kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza Zanzibar.

“Katika kipindi hiki kifupi tangu aingie madarakani, sote tumeshuhudia dhamira na azma yake njema ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar. Kupitia mwanzo huu mzuri aliouonesha, binafsi ninaamini tayari wananchi tumeshaona nuru ya kiongozi wetu huyu. Hivyo, nasi hatunabudi kumuunga mkono ili aweze kutimiza ndoto yake ya kujikwamua kiuchumi. Hakika “Yajayo Yanafurahisha”

Awali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kassim Ali alisema kukamilika kwa barabara hiyo kutaboresha maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa mkoa wa Kaskazini Unguja pamoja na mikoa jirani.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na ujenzi wa barabara ili kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji, hivyo aliwaomba wananchi wahakikishe wanailinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

ADVERTISEMENT
Mhariri

Mhariri

Related Posts

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais
HABARI

Dkt.JPM ampongeza Mseveni kushinda Urais

by Ombeni Osward
Jan 16, 2021
0

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania...

Read more
Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Raia wa Kenya ashikiliwa na TAKUKURU kwa kujaribu kumhonga apatiwe cheti cha COVID 19

Jan 16, 2021
Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Nyumba 6 zaezuliwa na upepo mkali ulioambata na mvua mkoani Njombe

Jan 16, 2021
Mseveni ashinda Urais tena

Mseveni ashinda Urais tena

Jan 16, 2021
Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Bilioni 11 zaokolewa chakula cha Wafungwa

Jan 16, 2021
Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Waziri Ndugulile awataka wakuu wa Taasisi zilizochini yake kuwa wabunifu ili kuleta mafanikio

Jan 16, 2021
Next Post
Jeshi la Ghana laingilia kati ugomvi ulioibuka Bungeni

Jeshi la Ghana laingilia kati ugomvi ulioibuka Bungeni

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

January 2021
M T W T F S S
« Dec    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In