Benki ya NMB Yafungua Tawi SUA – Morogoro – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home BIASHARA

Benki ya NMB Yafungua Tawi SUA – Morogoro

I am Krantz by I am Krantz
Feb 25, 2021
in BIASHARA
0 0
0
Benki ya NMB Yafungua Tawi SUA – Morogoro
0
SHARES
37
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB SUA’ katika Chuo Kikuu Cha Sokoine Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa wanasafiri umbali wa kilomita 6 kwenda matawi ya mjini Morogoro kupata huduma za kibenki.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Makamu Mkuu wa Chuo Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda – amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua tawi maeneo hayo na chuoni hapo ambapo anaamini, litachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo.


Makamu Mkuu wa Chuo Cha SUA – Prof. Raphael Chibunda akikata utepe kuzindua rasmi Tawi la NMB SUA. Wakishuhudia kutoka kulia kwake ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa NMB- Dismas Prosper, Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB – Emmanuel Akonaay na Meneja wa Tawi la SUA – Witness Mwanga
.

Chibunda alisema kuwa Benki hiyo licha ya kukuza uchumi pia itawapunguzia gharama, wateja wake

hususani wafanyakazi wa SUA, wanafunzi na wakazi wa Magadu, Mzinga, Kididimo,Misufini, Vibandani, Kasanga, Lugala na Mafiga waliolazimika kusafiri hadi Tawi la Wami zaidi ya kilometa  6 kupata huduma za kibenki- kwani sasa watapata huduma hizo kwa ukaribu zaidi.  

Naye Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, alisema kufungua tawi hilo litawanufaisha wateja wao ambao ni wanafunzi na wana Morogoro kuweza hufurahia huduma bora za benki hiyo ikiwemo, akaunti ya Mwanachuo, NMB Mkononi, Akaunti ya Fanikiwa, Huduma za bima ikiwemo Dunduliza, akaunti za kilimo na nyingine nyingi.

Ufunguzi wa tawi hili, unafanya Morogoro kuwa na matawi ya NMB 14 na Kanda ya Mashariki matawi 22 na jumal ya matawi 227 nchi nzima!

Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya hosipitali ya SUA na madawati kwa Shule ya Sekondari SUA vyote vikiwa na thamani ya Sh. 13.7 milioni ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.

Uongozi wa Benki ya NMB ukikabidhi vifaa vya hospitali kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu SUA – Prof. Raphael Chibunda pamoja na daktari wa hospitali ya SUA.

Makabidhiano ya Madawati kwa Shule ya Sekondari SUA.

I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

NMB yazindua Bima ya simu za mkononi
BIASHARA

NMB yazindua Bima ya simu za mkononi

by I am Krantz
Apr 19, 2021
0

 Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi(kulia) na...

Read more
Tigo yaungana na TAPSOA kuwezesha wateja kufanya malipo ya mafuta kwa Tigo Pesa

Tigo yaungana na TAPSOA kuwezesha wateja kufanya malipo ya mafuta kwa Tigo Pesa

Apr 16, 2021
Mawakala wa Tigo Pesa washinda mamilioni

Mawakala wa Tigo Pesa washinda mamilioni

Apr 15, 2021
Zantel yazindua ofa ya mfungo wa Ramadhan

Zantel yazindua ofa ya mfungo wa Ramadhan

Apr 15, 2021
Vodacom yashirikiana na Britam Tanzania kuzindua VodaBima kupitia M-Pesa

Vodacom yashirikiana na Britam Tanzania kuzindua VodaBima kupitia M-Pesa

Apr 13, 2021
Bolt yazindua Web App kupanua huduma za usafiri Tanzania

Bolt yapokea uwekezaji wa Euro 20 milioni kutoka IFC

Apr 11, 2021
Next Post
VIDEO; Wananchi waonesha Hamasa ya kushiriki Tigo Green For Kili

VIDEO; Wananchi waonesha Hamasa ya kushiriki Tigo Green For Kili

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

February 2021
M T W T F S S
« Jan   Mar »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In