Tigo yarahisisha malipo kwa wakulima 8,000 wa Chai nyanda za juu Kusini – Mwanaharakati Mzalendo
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
Home HABARI

Tigo yarahisisha malipo kwa wakulima 8,000 wa Chai nyanda za juu Kusini

Ni kupitia huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa ambayo ni salama na ya uhakika zaidi.

I am Krantz by I am Krantz
Feb 8, 2021
in HABARI
0 0
0
Tigo yarahisisha malipo kwa wakulima 8,000 wa Chai nyanda za juu Kusini
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini,Aidan Komba Akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigopesa kwa wakulima wa kilimo cha chai Rungwe mapema wiki iliyopita.




Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini,Aidan Komba Akifanua jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya Tigopesa kwa wakulima wa kilimo cha chai Rungwe mapema wiki iliyopita mkoani Mbeya.


Mwenyekiti wa Umoja wa wakulima wa chai wilayani Rungwe Andrew Mwendamanie akimshukuru Mkurungezi wa Tigo nyanda za juu kusini kwa kuwasogezea huduma ya malipo kwa njia ya Tigo 


• Ni kupitia huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa ambayo ni salama na ya uhakika zaidi.
Mbeya.Februari 6,2021. Kampuni ya Tigo Tanzania imeingia kwenye makubaliano na Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe ili kurahisisha malipo ya mazao yao kupitia simu maalumu kwaajili ya wakulima 8,000 katika Wilaya za Rungwe (Tukuyu), Busokelo na Kyela mkoani Mbeya.
Huduma hiyo ijulikanayo kama ‘Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa’ ni njia ya kinubinfu ya kutuma na kupokea pesa ambayo inayopatikana kupitia huduma ya kifedha ya Tigo, Tigo Pesa.
Akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa, Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini,Aidan Komba alisema “Tunafuraha sana kuungana na Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe kupitia huduma ya Malipo ya Chai kwa Tigo Pesa ambayo itatoa suluhu la kudumu la malipo na mahitaji ya kila siku ya kifedha kwa wakulima wa chai.”
Akifafanua namna huduma hiyo inafanya kazi,Komba alisema kwanza wakulima wanatakiwa kujisajili kupitia Umoja huo ili kuweza kunufaika na huduma hiyo ambapo pia watapewa taarifa juu ya ukusanyaji, usafirishaji,minada na mauzo ya mazao yao.
Mara baada ya fedha za mauzo kuingizwa kwenye akaunti ya Chama (Umoja wa wakulima) Tigo Pesa kupitia huduma ya Malipo ya Chai itatuma pesa moja kwa moja kwa wakulima ambao wamesajiliwa kwenye huduma hiyo na watapata  Ujumbe mfupi SMS papo hapo.
Baada ya kupokea fedha wakulima watakuwa na uhuru wa kutoa, kutuma au kufanya miamala mingine waipendayo kwa njia ya Tigo Pesa iliyo na mawakala kote nchini.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Lebi Hudson alisema “Tunapenda kuwashukuru sana Tigo Tanzania kwa kuhakikisha Umoja wetu unaingia kwenye mfumo wa fedha kidigitali (cashless). Wakulima wengi walikuwa wamezoea kutembea na pesa taslimu njia ambayo si salama hasa kwa kipindi ambacho tunakuwa tumepokea malipo ya mazao yetu.”


Zaidi ya wakulima 8,000 kwa mara ya kwanza hawatakuwa na wasiwasi kuhusu kuhusu malipo ya mazao yao.Huduma hii itawapa uhuru wa kupokea pesa na kutoa mahala popote nchini na kuwawezesha kufanya miamala kupitia Tigo Pesa huduma ya Tigo yenye mtandao mpana na wenye mawakala nchi nzima.

 Mwisho//

— 
 

I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe
HABARI

SIMULIZI; Nilivyolinda Familia Yangu Isikamatwe Wakati Wakitengeneza Pombe

by I am Krantz
Feb 26, 2021
0

Nilizaliwa katika familia masikini sana na wakati...

Read more
Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Dkt. Ndungulile afurahishwa na huduma ya kufungua akaunti kidijitali kupitia SimBanking

Feb 26, 2021
Auto Draft

FAINALI NMB MASTABATA WIKI IJAYO, 424 WAZOA ZAWADI

Feb 24, 2021
Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Mamia wajitokeza kujisajili na Mbio za Kili Marathon Jijini Dar Es Salaam

Feb 23, 2021
BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

BODI YA USAJILI WA WABUNIFU MAJENGO YAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA FANI HIYO

Feb 23, 2021
Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Wateja wa Vodacom kuvuna Shilingi 4.1 bilioni za faida ya kutumia M-Pesa.

Feb 23, 2021
Next Post
Musukuma amuomba Rais Magufuli kukutana na wafanyabiashara nchini

Musukuma amuomba Rais Magufuli kukutana na wafanyabiashara nchini

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

I agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.

Currently Playing

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

February 2021
M T W T F S S
« Jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In