ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

BoT yapongeza Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidijitali NMB

I am Krantz by I am Krantz
Oct 22, 2021
in HABARI
0
BoT yapongeza Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidijitali NMB
0
SHARES
225
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

 

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk.  Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya  NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Mkaguzi Mkuu  wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa, wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

 

RelatedPosts

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Waziri Dkt. Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Jan 25, 2023

🔴 #LIVE : NMB AWARDS SHOWCASE – NOV 23, 2022

Nov 23, 2022

NMB yapongezwa kusaidia Wakandarasi- Zanzibar

Nov 16, 2022
Load More
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk.  Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede (kati kati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya  NMB, Ruth Zaipuna wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya Tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

 

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dk.  Bernard Kibesse , Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dk. Edwin Mhede(kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya  NMB, Ruth Zaipuna na Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia  na Mabadiliko ya Kidigitali wa NMB, Kwame Makundi wakipata maelezo ya suluhishi mbali mbali za mifumo ya kifedha ya tehama kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni changa ya tehama, katika uzinduzi wa mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB.

 

 Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha(kushoto) na Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa NMB Emmanuel Akonaay, ni miongoni ya waliohudhuria uzinduzi wa  mfumo wa majaribio ya kidigitali wa NMB uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City – Dar es Salaam.

 

 

 

 

Benki ya NMB imezindua Mfumo wa Majaribio ya Suluhishi za Kidijitali (Sandbox Environment), ikiutengea Sh. Bilioni 1 za kusaidia bunifu zitakazopita, Mfumo ambao umepongezwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, na kutaka Taasisi za Fedha nchini kuiiga NMB katika kuleta njia mbadala za kutoa suluhu za kibenki ambazo ni rahisi, haraka na salama.

 

NMB Sandbox ni jukwaa huru la NMB linalotoa fursa kwa wabunifu wa Kidogitali na wabunifu binafsi wa Kitanzania kutumia Mifumo ya benki ya NMB kujaribu suluhishi zao kabla ya kuanza kutumika rasmi.  

ADVERTISEMENT

 

Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo Mgeni rasmi Dk. Kibesse alisisitiza kuwa mabenki nchini hayana budi kuendana na kasi ya mabadiliko ya tekinolojia ili kutoa suluhishi za huduma za kibenki, hasa katika nyakati hizi, ambazo tekinolojia  imetanua wigo wa kuhudumia.

 

“Uzinduzi huu wa Sandbox Environment, unafungua fursa kwa Kampuni changa na wabunifu binafsi kuonyesha ujuzi wao na kubuni suluhishi zitakazopunguza gharama za kibenki kwa watu wote, sambamba na kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania.

“BoT inatambua changamoto zinazo wakabili wateja wanapotumia huduma za kibenki, zikiwemo upatikanaji hafifu wa huduma hizo, ufinyu wa njia za kufikisha, gharama na uelewa mdogo walionao katika masuala ya fedha. 

“Serikali kupitia BoT imechukua hatua mbalimbali kumaliza changamoto hizo na uzinduzi huu unaashiria kuwa NMB inaunga mkono jitihada hizo, Kama ilivyofanya kutenga Sh. Bilioni 100 za mikopo nafuu kwa wakulima, wafugaji na wavuvi,” alisema Dk. Kibesse, akiahidi kuwa BoT itaendelea kushirikiana na NMB katika kuboresha sera zinazotoa mwongozo na kurahisisha ufanyaji wa biashara kwenye sekta ya kibenki.

 

Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alisema benki yake imejidhatiti na kujipambanua kuendana na kasi ya tekinolojia kwa kuleta suluhishi mpya zinazorahisisha  huduma za kibenki kwa mteja mmoja mmoja na wafanya biashara wadogo na wa kati, na kwamba benki yake imetenga kiasi cha Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuziwezesha suluhishi zitakazopita katika majaribio hayo.

ADVERTISEMENT

 

Zaipuna alimhakikishia Dk. Kibese kuwa, licha ya kwamba utatumika kwa majaribio, lakini Sanbox Environment hautoathiri kwa namna yoyote usalama wa taarifa, amana na faragha za wateja wao na kwamba baadhi ya tuzo za miaka ya karibuni ilizopata benki hiyo zimetokana na uwekezaji mkubwa waliofanya katika mifumo ya Kidijitali. 

 

“Hivi karibuni tumeshinda Tuzo ya Benki Bora ya Ubunifu ya wateja binafsi kutoka Jarida la Kimataifa la International Banker, huku tukiendelea kuongoza sokoni katika kutoa huduma za kibenki kidijitali na kuongeza bunifu Kama hizi za kuwaleta karibu wateja wetu kupitia mifumo ya kiteknolojia.

 

“Tunaahidi kuendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha tunafikisha na kuchagiza matumizi ya huduma za kifedha miongoni mwa Watanzania bila kujali walipo, yote yakiwezeshwa na bunifu hizi za Kidijitali,” alisema Zaipuna na kubainisha kuwa Sandbox Environment ni jukwaa muafaka kwa Kampuni za Ubunifu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kufanya majaribio ya bunifu zao.

Related

Tags: NMB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE
HABARI

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
HABARI

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC
HABARI

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI
HABARI

MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI
HABARI

MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA
HABARI

WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
October 2021
M T W T F S S
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031
« Jun   Dec »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In