ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Wednesday, July 6, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Amfuata Mwanamke Sweden Kutoka India kwa Baiskeli

I am Krantz by I am Krantz
Dec 14, 2021
in #CHUKUAHII, HABARI
0
Amfuata Mwanamke Sweden Kutoka India kwa Baiskeli
0
SHARES
62
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Pradyumna Kumar “PK” Mahanandias alizaliwa mwaka 1949 katika kijiji kimoja huko India kwenye moja ya matabaka ya kihindi ya chini kabisa (untouchables) kwahiyo hakuwa na tumaini la kutoka kwenye maisha ya ubaguzi na umaskini.

RelatedPosts

Jul 6, 2022

Jul 6, 2022

Jul 6, 2022
Load More

Ni kawaida Kwa wahindi kuita wanajimu watoto wanapozaliwa. Mnajimu alivyoitwa alisema huyu atakuwa mtu wa Sanaa ya uchoraji. Akikua hatachaguliwa mke kama watu wengine huko India. Huyu mtoto mke wake atatoka nchi ya mbali na atakuwa na nyota ya Taurus, atakuwa mmiliki wa msitu na atakuwa mwanamuziki anayecheza filimbi (flute).

Kweli PK alikuwa mchoraji mzuri hadi akapata scholarship kwenda kusomea chuo Cha Sanaa huko India. Kwa miaka mitatu alikuwa akikaa mitaani na kuchora watu na kupata pesa. Lakini hiyo ilikuwa hairuhisiwi kwahiyo saa zingine polisi walikuwa wanamchukua wanamweka nje ya kituo Cha polisi akae hapo.

Huko alikutana na watu wengi matajiri na maarufu kama Mahatma Gandhi.

Jioni moja ya mwaka 1975, mwanamke mwenye nywele ndefu za njano (blonde) na macho makubwa ya mviringo ya blue alimfuata akamuomba amchore. Anasema mwanamke yule alivyomsogelea alikosa nguvu hawezi kuelezea.

ADVERTISEMENT

Akasema huyu lazima nimtendee haki kwa urembo wake. Akajaribu kumchora akashindwa. Alikuwa anatetemeka. Akamuuliza huyo mwanamke unaweza kuja kesho? Huyu dada alirudi mara tatu na alichorwa mara tatu.

PK anasema alivyorudi mara ya pili alihisi huyu ndo yule mwanamke aliyetabiriwa. Akamuuliza wewe nyota yako ni Taurus? Binti akajibu ndio. Akamuuliza unamiliki msitu? Ndio. Unacheza filimbi? Binti akasema Ndio napenda kucheza filimbi na piano.

Akamwambia kwa shauku kubwa “Hii ilipangwa mbinguni! Ilikusudiwa tukutane!”

Binti akamuuliza we umejuaje? Akamwambia kama huamini nitakuonyesha Horoscope yangu iliyoandikwa nilipozaliwa. Wewe utakuwa mke wangu!

Yeye mwanamke (Charlotte) anayetoka Sweden anasema tangu akiwa mdogo alikuwa anatamani sana kwenda India. Kulikuwa na mwalimu alikuwa akiwaonyesha filamu za kihindi. Kadri alivyokua alikutana na wahindi wengi na kujifunza mengi kuhusu tamaduni zao. Aliwahi kwenda kwenye maonyesho fulani akaona ngoma ya kihindi kutoka mji aliozaliwa PK, akapumbazwa akili (hypnotized).

PK alivyomuambia kuwa atakuwa mke wake akakubali kwenda naye nyumbani kwa kina PK kuwaona ndugu zake. Anasema alijihisi nyumbani. Aliwapenda naye walimpenda. Anasema kama unaamini viumbe huzaliwa upya (reincarnation), basi yeye anaamini kabisa kuwa aliishi India zamani.

PK na Charlotte walioana na kuwa pamoja kwa muda wa wiki 3 tu kisha Charlotte akarudi Sweden. Hawakuonana mwa mwaka mmoja na nusu, zaidi ya kuwasiliana Kwa barua. Charlotte alitaka kumlipia ndege warudi wote lakini PK alikataa, alitaka ajilipie mwenyewe. Baada ya mwaka na nusu PK aliuza Kila kitu chake na kununua baiskeli.

Akaanza safari kutoka India Hadi Sweden Kwa baiskeli, umbali wa maili 4000 (6400km). Huko njiani alipata lift za maroli, alipata watu wa kumkaribisha kulala majumbani mwao, na alikuwa na “sleeping bag” aliyolalia nje akikosa pa kulala.

Alipitia Afghanistan, Iran, Turkey, Bulgaria, Yugoslavia, Germany, Austria na Denmark kufika Sweden.

Njiani aliendelea kupata barua kutoka kwa Charlotte. Alipata barua akiwa Afghanistan na Uturuki.

Anasema alikutana na watu wengi ambao walimfundisha mengi. Ilikuwa wakati wa tofauti sana maishani mwake. Ilikuwa ulimwengu wa Upendo, amani na uhuru. Shida pekee ilikuwa mawazo yake, mashaka yake.

Wamekuwa pamoja zaidi ya miaka 44 na kupata watoto wawili.

ADVERTISEMENT

PK anasema penye nia pana njia. Uoga na mashaka ndo adui wakubwa wanaofanya maisha yetu yawe magumu. Na anasema ndoa ni muunganiko si tu wa kimwili bali wa kiroho. Na siri ya ndoa yake ya furaha ni kupaki “ego” nje ya nyumba.

Pia anasema aliamini sana utabiri wa yule mnajimu na sasa anaamini matukio yote duniani yamepangwa

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

HABARI

by Pastory Kimaryo
Jul 6, 2022
HABARI

by Pastory Kimaryo
Jul 6, 2022
WIVU WA MAPENZI CHANZO CHA MAUAJI KIGOMA
HABARI

WIVU WA MAPENZI CHANZO CHA MAUAJI KIGOMA

by Shabani Rapwi
Jul 6, 2022
RIHANNA BILIONEA WA KIKE MDOGO ZAIDI
HABARI

RIHANNA BILIONEA WA KIKE MDOGO ZAIDI

by Shabani Rapwi
Jul 6, 2022
KISWAHILI LUGHA RASMI UGANDA
HABARI

KISWAHILI LUGHA RASMI UGANDA

by Shabani Rapwi
Jul 6, 2022
RICHARLISON AFUNGIWA NA KUPIGWA FAINI
HABARI

RICHARLISON AFUNGIWA NA KUPIGWA FAINI

by Shabani Rapwi
Jul 6, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2021
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Oct   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In