ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, December 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB yatunikiwa Tuzo ya Ubora

I am Krantz by I am Krantz
Dec 14, 2021
in HABARI
0
Benki ya CRDB yatunikiwa Tuzo ya Ubora
0
SHARES
371
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
Meneja Mipango ya Biashara wa Benki ya CRDB, Masele Msita (wa pili kulia)akipokea tuzo ya ubora kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya (ESOR), Edward Ryner katika hafla ya utoaji tuzo hizo iliyofanyika katika Hoteli ya Dusit Thani jijini Dubai, Falme za Kiarabu. Wengine pichani ni Balozi wa Tanzania nchini Falme za Kiarabu, Mohamed Mtonga (katikati), Meneja Mwandamizi Wawekezaji CRDB, Anna Mwasha (wa pili kushoto) na Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji wa Kijamii wa Benki hiyo, Joycelean Makele (kushoto) wakionyesha cheti cha mafanikio ya ubora.
 
==========    ==========     ==========

Mwaka 2021 unaisha vizuri kwa Benki ya CRDB ikiwa imetunukiwa tuzo tano ikiwamo ya ubora iliyotolewa mwishoni mwa wiki na Taasisi ya Utafiti wa Ubora barani Ulaya (European Society for Quality Research-ESQR).

Benki hiyo imekuwa pekee ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kushinda tuzo kutoka taasisi hiyo inayoheshimika duniani kwa utafiti unaohusisha masuala ya ubora wa huduma na bidhaa. Akipokea tuzo hiyo katika Hoteli ya Dusit Thani jijini Dubai,Falme za Kiarabu, Meneja wa Mipango ya Biashara wa Benki ya CRDB. Masele Msita alisema ni heshima kubwa kwao kutambulika kwa ubora jambo linaloongeza imani kwa wateja na wadau wao wengine.
“Ubora ni sehemu ya uti wa mgongo wa benki yetu. Tunafurahi kupata tuzo hii kutoka ESQR inayoenda sambamba na matamanio yetu. Inathibitisha maono ya benki kubuni huduma bora na kuzifanya zipatikane kwa urahisi kwa wateja,” alisema Msita.Meneja huyo alisema wakati wote benki ya CRDB inasisitiza na kuhamasisha ubora wa huduma na bidhaa inazotoa kwa wateja na wadau wengine inaoshirikiana nao katika ujenzi wa Taifa.

“Tunatimiza hili kwa kuimarisha mifumo yetu ya ndani,” alisema msita kwenye hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyohudhuriwa na wawakilishi wa mashirika na kampuni zilizoshinda kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya, Asia, Amerika na Australia.
 
Akiipongeza Benki ya CRDB kwa tuzo hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa ESQR, Edward Ryner alisema tuzo wanazotoa ni nembo ya uhakika wa ubora kwa wadau wa shirika au kampuni na huhamasisha menejimenti kuchukua hatua madhubuti kuendelea kuimarisha ubora kwa ajili ya wateja wake na wadau wengine.

Tuzo hii inaitambulisha Benki ya CRDB kuwa mzingatiaji mzuri wa maadili ya huduma kwa umaahiri mkubwa. Inaonyesha jinsi benki inavyojitofautisha sokoni kwa kubuni huduma salama za kidijitali,”alisema Ryner.
 
Tuzo hiyo inakuwa ya sita kwa Benki ya CRDB kushinda mwaka huu kwani ilishai buka mshindi wa kwanza wa tuzo ya uandaaji wa taarifa za fedha (FiRe)halafu ikawa benki bora ya tuzo za Bodi Taifa ya ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).

 
Tuzo nyingine ni benki bora yenye ubu-nifu Tanzania iliyotolewa na Jarida la Global Finance,benki bora inayokidhi matarajio ya wateja wake iliyotolewa na PANFinance pamoja na benki bora katika ubunifu wa kidijitali ya Consumer Choice Awards.

Benki ya CRDB ni miongoni mwa benki kubwa ya kizawa ambayo ina matawi nchini Burundi na inajipanga kufungua mengine katika Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC)pamoja na Sudan Kusini siku chache zijazo.

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!
HABARI

Tuliishi maisha ya shida sana kisa uchawi wa jirani!

by I am Krantz
Nov 30, 2023
EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga
HABARI

EACOP Yakamilisha Utaratibu Wa Fidia Kwa Kukabidhi Nyumba Ya 339 Mkoani Tanga

by I am Krantz
Nov 29, 2023
MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.
HABARI

MAWAKALA WA USAJILI WA VODACOM TANZANIA WATEMBELEA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA UTENDAJI BORA WA KAZI.

by I am Krantz
Nov 29, 2023
NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia
HABARI

NMB, Oryx Tanzania wazindua ‘Moto Mkali Bei Poa,’ kukopesha gesi ya kupikia

by I am Krantz
Nov 27, 2023
Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania
HABARI

Kampeni Ya Serengeti Maokoto Ndani Ya Kizibo Yazidi Kusambaza Furaha Kwa Watanzania

by I am Krantz
Nov 27, 2023
NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿
HABARI

NMB Mlipa Kodi Mkubwa na Bora Zaidi Tanzania 2023 🇹🇿

by I am Krantz
Nov 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TWEETS

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
December 2021
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Oct   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In