Na mwandishi wetu
Fainali ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Mpira wa Mikono inatarajia kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa Dar Es Salaam.
Fainali ya wanaume itawakutanisha Sereals watavaana dhidi ya Polisi Rwanda, huku mshindi wa tatu Ngome watamenyana dhidi ya Black Mamba.
Akizungumza kuhusu fainali Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA) Michael Chibawala,amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika .
“Timu zilizofika fainali nazitakiwa mchezo mwema na kwani kila mmoja tumeona uwezo wao na timu bora ,hivyo matarajiio kuona mchezo wa burudani na nidhamu ya kutosha na baadaye bingwa kupatikana,” amesema Chibawala.
Amewaita mashabiki na wapenzi wa mpira huo kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani ya fainali ya mchezo huo.
Sambamba kutarajia kumalizika kwa mashindano hayo ameomba wadau kujitokeza kuunga mkono maandalizi ya timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 18 ambayo inatarajia Kushiriki Michuano ya Kanda ya Tano 2022.
Amesema timu hiyo inatarajia kuingia kambini Januari 5 kwa ajili ya kujiandaa kuelekea katika mashindano ya Kimataifa.
@@@@@