Na mwandishi wetu
BONDIA Selemani Kidunda ameahidi kuibuka na ushindi dhidi ya Bondia Eric Tshimanga Katompa katika pambano la Ubingwa wa dunia wa WBF.
Pambano hilo la raundi 10 la uzito 76 limepangwa kufanyika Desemba 26 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza,Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Kidunda amesema anataka kuonesha ulimwengu na watanzania kuwa hakuna bondia anayeweza kuja kushinda ndani ya ardhi ya Tanzania.
Kidunda amesema, anataka kuwaonesha ladha watanzania na ushindi upo kikubwa ni kuungwa mkono kutoka na watanzania wote katika pambano hilo muhimu.
“Nimejiandaa vizuri, ushindi upo na kikubwa ni kusubiri siku ya pambano ifike na hatatoka na ushindi wowote,” amesema Kidunda
“Nia ya ushindi ipo na na nitampiga Kamtopa kwa namna yoyote, kwa staili yoyote hatatoka kikubwa ni sapoti kutoka kwa watanzania,” amesema
Kwa upande wa muandaaji wa pambano hilo kutoka Peaktime Media, Kapteni Selemani Semunyu amesema maandalizi yanakwenda vizuri hadi sasa.
Amesema, pambano hilo litakuwa la kulipa kisasi baada ya mpinzani huyo kumchapa Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ na kuondoka na Ubingwa.
“Nawashukuru sana wadhamini wote pia mnadhimu Mkuu wa Jeshi kwa kulisimamia pambano hili kuanzia mwanzo hadi mwisho na kusema ukweli bila yeye pambano hili lilikua na hatihati ya kufanyika,”.
Semunyu amesema, kabla ya pambano hilo kutakuwa na mapambano 10 ya utangulizi na sita yatakuwa ya kimataifa.
Ametaja Ismail Galiatano atavaana dhidi ya Denis Mwale, huku Ibrahim Class atamenyana dhidi ya Israel Kamwamba,likifuatia na George Bonalacha atapigana dhidi ya Hassan Milanzi.
Wengine Pali Magesta atavaana dhidi ya Oscar Richard na Viguli Shafii watamenyana dhidi ya Ally Kilongola.
Hamis Kibodi atapigana dhidi ya Iddy Jumanne, na Daniel Materu atavaana dhidi ya Haruna Swanga, wakati wanawake Grace Mwakamela atavaana dhidi ya Ruth Chisale, huku Najma Isike atapanda ulingoni dhidi ya Leila Zayidu.
@@@@@