Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Juma Kimori (katikati), Meneja Mwandamizi Idara ya biashara za kadi wa Benki ya NMB – Manfred Kayala (kushoto) na Mchambuzi wa masuala ya Kadi na Fedha, Helga Loth wakizindua rasmi Kampeni ya MastaBata Kivyakovyako msimu wa tatu 2021
Benki ya NMB imezindua msimu wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Kadi na Masterpass QR iitwayo ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako,’ ambako imetenga kiasi cha Sh. Mil. 240 zitakazo shindaniwa katika kipindi cha wiki 10.
Tangu mwaka 2018, NMB imekuwa ikiendesha kampeni za MastaBata kuchagiza matumizi ya kadi za NMB Mastercard na Masterpass QR miongoni mwa wateja wake.
Washindi wa kila wiki watajinyakulia TZS 100,000 na 1m/- kila mwezi. huku droo ya mwisho ikishuhudia washindi 30 wakishindia kila mmoja milioni tatu.
Mbali na kuhamasisha malipo ya kidijitali na kusaidia juhudi za kuifanya Tanzania kuwa uchumi usiotegemea sana pesa taslimu, pia NMB inaitumia kampeni hii kuwalipa fadhila wateja wake waaminifu.
Endelea kutumia Kadi yako ya NMB Mastercard au lipa kwa Masterpass QR kujiwekea nafasi ya kuwa mmoja wa washindi wa ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako