ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

RC MJEMA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI YA ‘PENDEZESHA TANZANIA’ KUPITIA BENKI YA CRDB

I am Krantz by I am Krantz
Dec 6, 2021
in HABARI
0
0
SHARES
279
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akiandaa mti kabla ya kuupanda wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  
amezindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB inayolenga kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Desemba 4,2021 katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga ambapo pia wananchi wamepatiwa miti bure kwa ajili ya kwenda kupanda kwenye maeneo yao.

Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuja na Programu ya Pendezesha Tanzania kwa kuhamasisha upandaji wa miti na utunzaji mazingira nchini kupitia kanda zake 7 za Kibenki.

“Kwa upande wa Kanda ya Magharibi mkoa wetu wa Shinyanga umebahatika kuwa chaguo la Benki ya CRDB kuendesha Programu hii kupitia kwenye viwanja vyetu vya maonesho ya Biashara na Madini vya Zainab Telack. Hadi leo katika viwanja hivi Benki ya CRDB wamekwisha panda takribani miti 1,000 na leo imekusudiwa kupandwa miti 900 ili kufikisha adhima yao ya kupanda miti 2,000. Naomba tuwapongeze”,amesema Mhe. Mjema.

“Napenda kuwashukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha Programu hii ya Kizalendo . Pia nawashukuru wadau wote mliojitokeza katika zoezi hili la upandaji miti. Napenda kuzihamasisha taasisi zote zilizopo mkoani Shinyanga kwa kuiga na kuunga mkono juhudi hizi ambazo wenzetu Benki ya CRDB wamezionesha kwa Programu yao ya PendezeshaTanzania kwa kupanda miti na kuhamasisha utunzaji mazingira”,ameongeza Mjema.

Mkuu huyo wa mkoa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za utunzaji mazingira na uwekaji wa mikakati ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi zilizopelekea kupata fedha za Mfuko wa Utunzaji Mazingira (GCF).

Mjema amesema Mkoa wa Shinyanga umejipanga kupanda miti Milioni 9 na sasa miti milioni 5 imepatikana tayari kwa kuanza kupandwa huku akiagiza Wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia upandaji miti na miti iliyopandwa.

Amefafanua kuwa dunia kwa ujumla inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi yanayochangiwa shughuli za kibinadamu hususani ukataji miti na ukuaji wa viwanda ambao unasababisha ongezeko la gesi ukaa hali inayosababisha ukosefu wa mvua za kutosha na zisizotabilika na ongezeko la joto na kuyeyuka kwa barafu katika Mlima Kilimanjaro.

“Kwa ujumla hali siyo nzuri, sisi sote ni mashahidi siku hizi hata msimu wa mvua haueleweki hivyo kusababisha mavuno hafifu, ukosefu wa maji ya uhakika. Mwarobaini wa haya ni sisi kuamua kwa dhati kutunza mazingira hasa kwenye vyanzo vya maji kwa kupanda miti na kuachana na ukataji miti ovyo kwa faida yetu pamoja na vizazi vijavyo”
,ameeleza.

“Wananchi wa Shinyanga tuhakikishe katika makazi yetu tunatunza mazingira na kupanda miti hususani miti ya matunda,vivuli na mbao ili kuifanya dunia iwe sehemu salama ya kuishi”,amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amesema tayari wilaya ya Shinyanga inaendelea na Kampeni ya Upandaji miti ya ‘Shinyanga ya Mikwaju na Miembe’ hivyo kuishukuru Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika upandaji miti na utunzaji mazingira.

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui wamesema wameanza Programu ya Pendezesha Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupanda miti na kutunza mazingira ili kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema lengo la Benki ya CRDB ni kupanda miti 2,000 katika viwanja vya maonesho ya Biashara na Madini vya Zainab Telack na tayari walishapanda miti 1,100 na leo wamepanda miti 900 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.

“Sisi Benki ya CRDB ni Mabalozi wazuri wa upandaji miti na utunzaji mazingira hivyo tumeanzisha Programu ya Pendezesha Tanzania ili kuonesha mfano kwa wananchi wawe na mwamko wa kupanda miti na kutunza mazingira. Tunawashukuru wadau wote ambao leo mmeungana nasi kushiriki zoezi hili la upandaji miti”,amesema Pamui.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwasili katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga kwa ajili ya kuzindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Maandishi yakisomeka ‘Pendezesha Tanzania: Karibu Uwanja wa Maonesho Butulwa Shinyanga, CRDB yaliyopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara na Madini wa Butulwa maarufu viwanja vya Zainab Telack uliopo kata ya Old Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akizungumza wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui. Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Erenestina Richard
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema.
Mkuu w wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini. Kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema, Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Saidi Pamui.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.  
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akiandaa mti kabla ya kuupanda wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akipanda mti wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema  akipanda mti wakati akizindua rasmi Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui akimwagilizia maji mti aliopanda wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkazi wa Old Shinyanga akiwa amebeba miti iliyotolewa bure kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati aliyevaa kofia) akipiga picha na wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (katikati) akipiga picha na wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (wa tatu kulia) akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) akifuatiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga , Zuwena Omary. Wengine ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney  (kushoto) akifuatiwa na Meneja Biashara Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda yaa Magharibi, Saidi Pamui baada ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Upandaji miti kupitia Programu ya Pendezesha Tanzania inayoendeshwa na Benki ya CRDB  ili kuhamasisha upandaji miti na utunzaji wa mazingira nchini.

Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2021
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Oct   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In