ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

RC SOPHIA MJEMA AKABIDHI MAGODORO KWA AJILI YA WAFUNGWA NA MAHABUSU GEREZA LA SHINYANGA

I am Krantz by I am Krantz
Dec 22, 2021
in HABARI
0
0
SHARES
139
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

MORGAN HERITAGE KUACHIA ALBUM YAO APRILI 21

Mar 24, 2023

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

Mar 24, 2023

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023
Load More
ADVERTISEMENT

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amekabidhi magodoro ili kukabiliana na uhaba wa malazi unaotokana na changamoto ya msongamano wa wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga.

Mhe. Mjema amekabidhi magodoro 50 kati ya 100 yaliyotolewa na Kampuni ya GSM leo Jumatano Desemba 22,2021 kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga ikiwa ni sehemu ya jitihada anazofanya katika kuondoa changamoto zilizopo kwenye magereza.


“Wafungwa wanakwenda gerezani kwa ajili ya kujifunza kutokana na makosa waliyofanya. Ni sawa wametenda makosa lakini kuwa gerezani haimaanishi kwamba wakose haki zao ndiyo maana serikali inaendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuondoa changamoto zilizopo magerezani na kutokana na hali hiyo nimefanikiwa kupata magodoro 100 kutoka Kampuni ya GSM, na leo nakabidhi magodoro 50 na mengine yatakuja ili yakatumike kuondoa changamoto ya malazi gerezani”,amesema Mjema.

“Msongamano katika gereza la wilaya ya Shinyanga ni mkubwa ambapo mahabusu na wafungwa wanafika takribani 450 na mkoa mzima idadi ni zaidi ya 800 hivyo ni lazima tufanye jitihada za kuhakikisha wanapata malazi. Naomba wadau wengine wajitokeze kutoa mahitaji mbalimbali kwenye magereza yetu ili waishi vizuri”,ameongeza Mjema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa jitihada anazoendelea kuzifanya kuondoa changamoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutatua changamoto ya msongamano magerezani.

“Hivi sasa tunaendelea na jitihada za kujenga bweni ‘sero’ mpya ya magereza yenye uwezo wa kubeba mahabusu/wafungwa 100. Naomba wadau wajitokeze kuchangia ujenzi huu pamoja na kuendelea kusaidia mahitaji mbalimbali katika magereza. Tumekuwa tukiona hata nyakati za Sikukuu wadau wamekuwa wakifika kwenye magereza na kutoa misaada na zawadi tunawashukuru sana, naomba tuendelee na moyo huo”,amesema Mboneko.

Akipokea Magodoro hayo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema kwa kufanikisha kupatikana kwa magodoro ambayo yatasaidia kupunguza changamoto ya malazi katika Gereza la wilaya ya Shinyanga ambalo lina msongamano mkubwa wa mahabusu na wafungwa.

Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya amesema gereza hilo lina uwezo wa kubeba wafungwa na mahabusu wa kiume 130 na wa kike 30 (jumla 160) lakini idadi imekuwa ikipanda hadi kufikia zaidi ya 450 ambapo leo Desemba 22,2021 wapo 439 huku akibainisha kuwa changamoto iliyopo kuwa ni malazi kwani magodoro ni machache.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga leo Jumatano Desemba 22,2021 katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Muonekano wa sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Muonekano wa sehemu ya magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga (kushoto) akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akikabidhi magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga  
 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Shinyanga Lazaro Nyanga (kushoto) na Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Shinyanga, William Makwaya wakikagua magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Shinyanga 

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Ijumaa Machi 24,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2021
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Oct   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In