Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya d.light, imezindua huduma ya manunuzi ya simu janja kwa mkopo.
Hii ni kwa kuzingatia umuhimu wa simu hizo katika kipindi hiki cha teknolijia ambapo Vodacom imeingia ubia na d.light kuhakikisha wateja wake wanapata fursa ya kutumia simu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,mkuu wa kitengo cha mauzo na usambazaji wa kampuni hiyo George Lugata amesema wamechukua uamuzi huo kwa lengo la kuendelea kuwaletea wateja wao huduma na bidhaa zenye tija na manufaa zaidi.
Lugata amesema kwa sasa matumizi ya simu janja yamekuwa makubwa na hivyo ni muhimu kuwawezesha wateja wake kupata fursa hiyo ya kutumia simu janja kwa kuwakopesha.
“Leo ninafuraha kubwa kuzindua huduma ya manunuzi ya simujanja kwa mkopo ambayo Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na d. Light inaleta kwa wateja wake.
Kama mnavyofahamu matumizi ya simujanja yameongezeka kwa kasi nchini. Lakini licha ya ongezeko hili bado takriban theluthi mbili kati ya tano hawatumii simujanja, ambapo kwa kutumia simu hizo, ndipo mtu anapata huduma za intaneti”,amesema Lugata.
Hata hivyo Lugata amesema miongoni mwa masharti ya mkopo wa kupata simu hizo ni pamoja na wateja wa Vodacom kutanguliza malipo ya awali ya Tsh 80,000, ambapo watalipa kiasi cha Tsh. 1,800 kwa siku kwa muda wa siku 300 ili kumaliza deni analodaiwa.
Aidha Vodacom, itatoa zawadi ya GB 96 kwa mwaka mzima, kwa wateja watakaonunua simu hizo lengo ikiwa ni kila mtanzania kuweza kumiliki simu janja.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya d.light Charles Natai, amasema kampuni yake imeungana na Vodacom kuhakikisha watanzania wa kipato cha chini wanaweza kumiliki simu janja.
“d.light inatoa bidhaa za bei nafuu kwa wateja wa kipato cha chini na ndiyo maana tyumeungana na Vodacom ili kuelekea katika msimu wa sikuu ya Krismas kila mtu aweze kumili simu janja”, amesema Natai.
Natai ameongeza kuwa endapo simu atakayonunua mteja itakuwa na hitilafu,kampuni hiyo itawapa namba wateja hao ili kuhakikisha zinafanyiwa marekebisho.
Simu zitakazotolewa na Vodacom ni aina ya Sumsum A02 zenye ukubwa wa inchi 6.5 ambapo mteja wa Vodacom atapata GB 8 kwa kila mwezi ndani ya mwaka mmoja.