ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

WATEJA T-PESA KUNUFAIKA NA USHIRIKIANO MPYA NA POSTA TANZANIA

I am Krantz by I am Krantz
Dec 8, 2021
in HABARI
0
WATEJA T-PESA KUNUFAIKA NA USHIRIKIANO MPYA NA POSTA TANZANIA
0
SHARES
309
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (wa pili kushoto) pamoja na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), kwa makubaliano hayo kwa sasa TPC inakuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO wa T-PESA.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (kushoto) pamoja na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (kulia) wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (katikati aliyesimama) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kwenye hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya T-PESA na Shirika la Posta Tanzaina (TPC), leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde (wa pili kushoto) na Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel (wa pili kulia) wakionesha nakala za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kibiashara baina ya pande mbili. Pembeni yao ni wanasheria wa pande zote mbili wakishuhudia.


RelatedPosts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

Mar 28, 2023

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Mar 28, 2023

TAIFA STARS YAAHIDI KUENDELEZA ILIPOISHIA

Mar 28, 2023
Load More

Na Mwandishi Wetu, Dar

KAMPUNI ya T-PESA imeingia makubaliano ya ushirikiano kibiashara na Shirika la Posta Tanzaina (TPC) unaolenga kurahisisha huduma za kifedha kwa mawakala pamoja na wateja wake.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mpango wa T-PESA kuboresha huduma zake za Kifedha nchini na kuhakikisha wateja wake wanakuwa karibu zaidi na mawakala na pia kupata huduma kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu.

Aidha alisema katika makubaliano hayo kwa sasa Shirika la Posta linakuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO. Alisema T-Pesa inatambua ukubwa wa Shirika la Posta na mchango wake katika kutoa huduma kwa wananchi, hivyo kitendo cha Posta kupewa nafasi hiyo ni chaguo sahihi kuwafikia mawakala wadogo na wateja hadi ngazi ya wilaya. 

“…Kwa nafasi ya kipikee napenda kuishukuru Menejimenti ya Posta chini ya Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Mbodo kwa kukubali Shirika la Posta kuwa WAKALA MKUU ambaye anaenda kubeba dhamana kubwa ya kuwahudumia MAWAKALA WADOGO. 

Tunatambua ukubwa wa Shirika la Posta na mchango wake katika kutoa huduma kwa wananchi. Tunahakika POSTA kuwa WAKALA MKUU ni chagua sahihi ya kuwafikia mawakala wadogo na wateja hadi ngazi ya Wilaya,” alisema Bi. Lulu Mkudde.

Aliongeza kuwa T-PESA inaendelea na uboreshaji wa huduma zake huku lengo likiwa ni kuhakikisha huduma zinapatikana kwa urahisi zaidi mahali popote na ndiyo haswa sababu ya kuendelea kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na taasisi zingine.

Akifafanua zaidi kwa wanahabari, Bi. Mkudde alibainisha kuwa muunganiko huo wa huduma za kibiashara baina ya taasisi hizo mbili unalenga kuwawezesha wananchi kufanya miamala yao ya Kifedha kwa njia rahisi na salama zaidi, ambapo sasa Wakala wa T-PESA atakuwa na uwezo wa kupata Floti kupitia POSTA ikiwemo huduma za Uwakala kwa Wateja kutoa pesa kwenye akaunti zao kupitia Ofisi za TPC.

“…Ili kufanikisha ukuaji wa huduma zitolewazo na T-PESA, mipango madhubuti imekuwa ikifanywa ikiwa ni pamoja na kuunganisha huduma zetu pamoja na benki mbalimbali ikiwemo CRDB, TCB, (zamani TPB), NMB, Peoples Bank of Zanzibar na AZANIA Benki ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zetu,” aliongeza Bi. Mkudde.

ADVERTISEMENT

Kwa upande wake, Kaimu Posta Masta Mkuu, Aron Samwel akizungumzia katika hafla hiyo alisema ushirikiano huo baina ya T-PESA na TPC utaleta tija kwa pande zote mbili kutokana na kwamba huduma zao zimesambaa nchi nzima na sasa huduma za T-PESA zitapatikana kila mahali zilipo huduma za Shirika la Posta.

ADVERTISEMENT

—

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE
HABARI

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
HABARI

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC
HABARI

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI
HABARI

MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI
HABARI

MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA
HABARI

WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
December 2021
M T W T F S S
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031  
« Oct   Jan »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In