ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, June 9, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

100 ‘WALAMBA’ MIL 10/- ZA WIKI YA PILI NMB MASTABATA

I am Krantz by I am Krantz
Jan 15, 2022
in HABARI
0
100 ‘WALAMBA’ MIL 10/- ZA WIKI YA PILI NMB MASTABATA
0
SHARES
120
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

KARIM BENZEMA ATAMBULISHWA RASMI AL-ITTIHAD

KARIM BENZEMA ATAMBULISHWA RASMI AL-ITTIHAD

Jun 9, 2023

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023

Jun 9, 2023

TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA

Jun 8, 2023
Load More

Ofisa Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Mary Mwasikili, akizungumza na mmoja wa wateja walioshinda katika droo ya pili ya Kampeni ya ‘NMB MastaBata Kivyako Vyako’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu).

Meneja Kitengo cha Kadi Benki ya NMB, Sophia Mwamwitwa, akibonyeza kitufe cha kompyuta kutafuta washindi wa droo ya NMB MastaBata Kivyako Vyako iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Afisa Kitengo cha Kadi Benki ya  NMB, Mary Mwasikili na kushoto ni Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Mfuru. (Na Mpiga Picha Wetu)

…………………………..

KAMPENI ya ‘NMB MastaBata – Kivyako Vyako’, inayoendeshwa na Benki ya NMB imeezidi kushika kasi ambako wateja 100 wa Benki hiyo wametangazwa washindi wa Sh. Milioni 10 za droo ya wiki ya pili.

NMB MastaBata ni kampeni inayolenga Kuhamasisha Matumizi na Malipo kwa njia ya MasterCard, Masterpass QR na PoS, ambako NMB imetenga zaidi ya Sh Mil. 200 zinazoshindaniwa katika kipindi cha wiki 10, huku washindi wakipewa pesa taslimu ili kuwapa uhuru wa kujipangia matumizi.

Akizungumza kabla ya droo ya Wiki ya Pili iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kitengo cha Kadi wa NMB, Sophia Mwamwitwa, alisema kampeni hiyo inapewa msukumo wa mahitaji ya ulimwengu wa kisasa unaoamini katika matumizi yasiyohusisha pesa taslimu, ambayo yanakabiliwa na changamoto kadhaa, zikiwamo za upotevu na wizi.

Aliongeza kuwa, kutokana na uhitaji huo, NMB wakabuni kampeni hiyo ambayo imefanyika kwa misimu mitatu sasa na kuchagiza ukuzaji wa matumizi ya kadi, kiasi cha benki yake kutunukiwa Tuzo ya Benki Kinara wa Uhamasishaji Matumizi ya Kadi mwaka 2021, ambako walikuza matumizi hayo kwa asilimia 104.

“Kampeni hii ilianzishwa mwishoni mwa Desemba mwaka jana na itaendelea kwa wiki 10, ambako zaidi ya washindi 1,000 watazawadiwa pesa taslimu. Tutakuwa na washindi 100 wa kila wiki, washindi 25 wa kila mwezi ambao watajishindia Sh. 100,000 kila mmoja, na katika ‘Grande Finale’ tutatoa washindi 30 wa Sh. Mil. 3 kila mmoja.

“Wito kwa wateja wetu ni kuendelea kutumia kadi zao kufanya malipo na matumizi kwa MasterCard, Masterpass QR na Vituo vya Malipo vya NMB (PoS), ili kujiongezea nafasi za kushinda. Wasio na kadi waziombe matawini na wasiokuwa wateja wetu, watembelee matawi yetu kote nchini wafungue akaunti, ili sio tu kushinda zawadi hizi, bali pia kufurahia huduma zetu,” alisema Mwamwitwa.

NMB MastaBata – Kivyako Vyako inafanyika chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ambapo droo ya pili ilikuwa ikisimamiwa na Pendo Mfuru, aliyewahakikishia wateja wa NMB kuwa vigezo na masharti vinazingatiwa katika kupata washindi wa kampeni hizo.

“Jukumu letu kubwa ni kusimamia michezo hii na niko hapa kwa jukumu hilo na niwahakikishie wateja wote kuwa kila kitu kinaenda chini ya utaratibu, sheria na kanuni za GBT,” alisema Pendo Mfuru kabla ya kuanza uchezeshwaji wa droo hiyo ya pili.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023
HABARI

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO JUNI 9, 2023

by ALFRED MTEWELE
Jun 9, 2023
TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA
HABARI

TRA YAUJUZA UMMA KUWA USAJILI WA TIN INAYOSISITIZWA NI KAMA NIDA, SIO ILE YA BIASHARA

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
DR. MPANGO ATILIA MKAZO JITIHADA ZA KULINDA HIFADHI YA BAHARI NA RASILIMALI ZAKE
HABARI

DR. MPANGO ATILIA MKAZO JITIHADA ZA KULINDA HIFADHI YA BAHARI NA RASILIMALI ZAKE

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
EWURA YATOA BEI HII KIKOMO YA MAFUTA NCHINI
HABARI

EWURA YATOA BEI HII KIKOMO YA MAFUTA NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI HUU LEO
HABARI

RAIS SAMIA AMEFANYA UTEUZI HUU MPYA LEO

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023
MESSI AFUNGUKA SABABU ZA KUIPOTEZEA BARCA
HABARI

MESSI AFUNGUKA SABABU ZA KUIPOTEZEA BARCA

by ALFRED MTEWELE
Jun 8, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In