ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB yazindua kampeni kuhamasisha Watanzania kutumia huduma na bidhaa bunifu za benki hiyo kufanikisha malengo yao 2022

I am Krantz by I am Krantz
Jan 3, 2022
in HABARI
0
Benki ya CRDB yazindua kampeni kuhamasisha Watanzania kutumia huduma na bidhaa bunifu za benki hiyo kufanikisha malengo yao 2022
0
SHARES
133
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

Mar 28, 2023

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

Mar 28, 2023

TAIFA STARS YAAHIDI KUENDELEZA ILIPOISHIA

Mar 28, 2023
Load More
ADVERTISEMENT
Benki ya CRDB imewataka Watanzania kutumia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki hiyo kwa makundi mbalimbali ya wateja kufanikisha malengo waliyojiwekea katika mwaka huu mpya wa 2022. Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Unachostahili ni CRDB Bank” inayolenga katika kutoa elimu na kuwaonyesha Watanzania fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki yao ya CRDB

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki ya CRDB ikiwa benki ya kizalendo inatambua kuwa inawajibu wa kuwasaidia Watanzania na wadau wengine wa maendeleo nchini kutimiza malengo katika mwaka huu mpya 2022. Nsekela alisema kupitia kauli mbiu yake ya “Benki inayomsikiliza mteja”, Benki ya CRDB imekuwa ikisikiliza na kufanyia kazi mahitaji ya wateja ili kuwapa wanachostahili.
“Mwaka jana tulifanya utafiti maalum kufahamu mahitaji halisi ya wateja ambayo yamekuwa yakibadilika kila uchwao, utafiti ule ulienda sambamba na kupokea maoni ya namna bora ya kuwahudumia wateja. Ninajivunia kusema tumeweza kufanyia kazi maoni ya wateja na kuboresha sehemu kubwa ya huduma na bidhaa zetu ili kuweza kuwapa wanachostahili,” amesema Nsekela.

Nsekela alisema moja ya maeneo ambayo Benki hiyo imeyafanyia maboresho ni katika mtandao wa ufikishaji huduma za kibenki ambao unajumuisha mifumo ya kidijitali ikiwamo SimBanking, CRDB Wakala, TemboCard, na Internet banking ambayo inawawezesha wateja kupata huduma popote pale walipo. Hivi sasa wateja wa Benki ya CRDB wanaweza kupata zaidi ya asilimia 90 ya huduma kupitia njia hizo mbadala za upatikanaji wa huduma.
“Tunatambua wateja wanahitaji muda mwingi zaidi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi, hivyo uboreshaji wa mifumo hii utawawezesha kufanya miamala yao kwa wakati na hivyo kuongeza ufanisi katika biashara na maeneo yao ya kazi hivyo kuongeza ufanisi,” amesema Nsekela huku akibainisha maboresho hayo yamesaidia kuongeza urahisi na unafuu wa kwa wateja.

Katika kampeni hiyo Benki ya CRDB pia imejipanga kuwaelimisha wateja juu ya huduma za uwezeshaji zinazotolewa na benki hiyo kupitia mikopo kwa makundi mbalimbali ya wateja ikiwamo wanafunzi, wafanyakazi, wajasiriamali, wakulima, wafanyabishara, makampuni na taasisi.  “Niwahakikishie kuwa Benki yetu ina uwezo mkubwa kimtaji unaowezesha kutoa mikopo kwa makundi mbalimbali kwa gharama nafuu, hivyo niwasihi Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo kufikia malengo yao.”
Nsekela alisema benki hiyo pia imejipanga kuendelea kushiriki kikamilifu katika miradi ya kimkakati ya Serikali huku akimpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza utekelezaji wa miradi hiyo. “Ukubwa wa mizania yetu unatufanya tuwe na uwezo mkubwa wa kushiriki katika kuwezesha wadau wote wanaoshiriki katika miradi hii ikiwamo Serikali yenyewe, pamoja na wakandarasi na wazabuni,” amesema Nsekela.

Aidha, Nsekela alieleza kuwa katika kipindi cha kampeni hiyo wateja pia watakuwa wakielimishwa juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba ili kufikia malengo kwa kutumia akaunti mbalimbali za benki hiyo. Benki ya CRDB ina akaunti zinazoongoza makundi mbalimbali ya wateja kuanzia akaunti za Junior Jumbo maalum ya watoto, wanafunzi – Scholar, wafanyakazi – Salary, wajasiriamali – Hodari, wafanyabiashara – Current, wakulima – FahariKilimo, Wanawake – Malkia na hata Wastaafu – Pension Account.

“Hizi ni baadhi tu ya fursa nyingi ambazo wateja na wadau wetu wanastahili ili kufikia malengo yao kwa mwaka huu 2022. Katika kipindi hiki cha kampeni tumejipanga kuhakikisha tunatoa huduma za daraja la kwanza kwa wateja wetu ili wawaeze kunufaika na fursa hizi zinazotolewa na benki yao.,” amesema Nsekela.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa amesema benki hiyo itaendelea kutekeleza ahadi yake ya kumuweka kwanza mteja na kuwakaribisha Watanzania wote, wateja binafsi, makampuni, na taasisi kuchangamkia fursa hizo kufikia malengo yao. “Benki yetu ni imara na yenye kuaminika kwa ubunifu hapa nyumbani na nje ya nchi. 

Nafikiri wote tumeona tulivyopokelewa vizuri hata nchi za jirani za Burundi na Congo, na inavyoaminika na Serikali kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye kusaidia kujenga uchumi,” alisema Tully huku akiwataka wafanyabiashara wanaofanya biashara nan chi za jirani pia kutumia fursa zinazotolewa na benki hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda aliwashukuru Watanzania kwa kuendelea kuichagua benki hiyo kuwa mtoa huduma wao na kuwaahidi benki hiyo itaendelea kuwapa wanachostahili kupitia bidhaa na huduma bunifu.

—

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE
HABARI

DC JOKATE MWEGELO AZURU NCHINI AFRIKA KUSINI KUTANGAZA FURSA ZAO LA MKONGE

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
HABARI

MBUNGE ATOA MAJIKO YA GESI 700 KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC
HABARI

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO NA WANAHABARI, JNICC

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI
HABARI

MFAHAMU MVUVI ALIYEPOTELEA BAHARINI SIKU 438, NA KUKUTWA BADO YUPO HAI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI
HABARI

MAKAMU WA RAIS MAREKANI ZIARANI KESHO NCHINI

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023
WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA
HABARI

WASANII BONGO WALIOTAJWA PLAYLISTS YA KAMALA

by ALFRED MTEWELE
Mar 28, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In