ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

TUNATAKA TTCL IWE KITOVU CHA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI – WAZIRI NAPE NNAUYE

I am Krantz by I am Krantz
Jan 28, 2022
in HABARI
0
TUNATAKA TTCL IWE KITOVU CHA MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI – WAZIRI NAPE NNAUYE
0
SHARES
166
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanya ziara yake ndani ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL – Corporation). Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya TTCL, Bw. Rajabu Uweje Yacoub pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL – Corporation, Bw. Waziri W. Kindamba wakifuatilia mkutano huo.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanya ziara yake ndani ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL – Corporation). Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya TTCL, Bw. Rajabu Uweje Yacoub pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL – Corporation, Bw. Waziri W. Kindamba wakifuatilia mkutano huo.


RelatedPosts

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mar 23, 2023

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

Mar 23, 2023
Load More

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nape Nnauye amefanya ziara ndani ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL – Corporation) na kubainisha kuwa lengo la wizara yake ni kuifanya taasisi hiyo kuwa kitovu cha mawasiliano kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

ADVERTISEMENT

Waziri Nnauye amebainisha hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea TTCL – Corporation na kuzungumza na menejimenti ya shirika pamoja na kupokea taarifa na changamoto zinazolikabili shirika.

“Tageti yetu ni kuifanya TTCL – Corporation kuwa shirika bora la mawasiliano kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tunataka tutafute njia ya pamoja ya kuliboresha shirika hili,” alisema Waziri huyo wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mh. Nnauye akizungumza na wanahabari.

Alisema katika ziara hiyo aliyoiita ya kujifunza wamepokea taarifa ambapo, yapo mambo yaliyowasilishwa kama changamoto ambayo yanakwamisha shirika hilo kufanya vizuri zaidi, hivyo kama wizara inayoisimamia inakwenda kukaa na kuyachakata kabla ya kuyatolea maelekezo.

“Tumeyapokea na tunaenda kukaa na kuyachakata, yanayopaswa kufikishwa mamlaka za juu tutayawasilisha na yaliyochini yetu tunaenda kuyafanyia kazi kisha baadaye tutatoa maelekezo  yetu ili kusonga mbele,” alifafanua waziri huyo.

“…Alitolea mfano kuwa zipo sheria za manunuzi ya umma ambazo TTCL imekuwa ikilazimika kuzifuata mchakato wake unaweza kuchukua hadi miezi sita, wakati sekta binafsi ambao ni washindani wa TTCL unaweza hata kuchukua siku mbili…sasa ukimwacha hapo kushindana na wenzake lazima ataachwa mbali,” alisema Waziri Nnauye.

ADVERTISEMENT

Aidha akifafanua zaidi alisema yapo baadhi ya mambo ya kimaamuzi ambayo TTCL haiwezi kufanya pekee hadi kushirikisha ngazi nyingine, jambo ambalo limekuwa kama changamoto kwenye shirika na kukwamisha baadhi ya mipango ya maendeleo ya shirika.

Aliongeza kuwa wamejipanga kukutana pia na wafanyakazi wa TTCL na kuzungumza nao ili kupata maoni na changamoto zao na kuangalia namna bora ya kushirikiana kuhakikisha shirika linasonga mbele kwa mafanikio zaidi. 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE
HABARI

YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE

by Shabani Rapwi
Mar 22, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In