ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Vodacom Tanzania Yakabidhi Gari Jipya la Tusua Mapene Ikiwa Sehemu ya Msimu wa Upendo

· Ni gari la kwanza la mshindi wa promosheni ya Tusua Mapene

I am Krantz by I am Krantz
Jan 4, 2022
in HABARI
0
Vodacom Tanzania Yakabidhi Gari Jipya la Tusua Mapene Ikiwa Sehemu ya Msimu wa Upendo
0
SHARES
319
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More
Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini, Mhe. Abbas  Kayanda (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mshindi wa gari jipya aina ya Suzuki S Presso kutoka promosheni ya Vodacom Tusua Mapene, Shemmy Chisumo funguo za gari baada ya kuibuka mshindi wa gari la kwanza la promosheni hiyo, hafla hii imefanyika kwenye viwanja vya Manyema, Mbuyuni wilayani humo. Sambamba na zawadi hiyo washindi sita walijishindia Tv za kisasa, na wengine kumi walijishindia Simujanja kutoka promosheni ya “Show Love, Tule Shangwe” zinazotolewa msimu huu wa sikukuu kwa wapendanao, ili ushinde  mteja unatakiwa kununua bando na kutumia huduma ya M-pesa, kushoto kwa mshindi ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania George Venanty aliyemwakilisha mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo.
Washindi wa zawadi za promosheni ya “Show Love,Tule Shangwe” wakiwa na zawadi zao mara baada ya kukabidhiwa kwenye hafla iliyofanyika katika viwanja vya Manyema Mbuyuni wilayani Moshi, jumla ya Tv sita za kisasa na simu janja kumi zilitolewa kwa wapendanao huku pia washindi wa pesa taslimu nao walikabidhiwa pesa walizoshida. Ili ushinde  mteja unatakiwa kununua bando na kutumia huduma ya M-pesa kwa kupiga *149*01#

·      Zawadi mbalimbali zimetolewa kwa washindi wa promosheni ya “Show Love, Tule Shangwe”

Moshi, 30 Disemba 2021 – Kampuni ya teknolojia na Mawasiliano inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa msimu wa furaha unaoitwa “Show Love, Tule Shangwe” pamoja na mshindi mkuu wa kwanza wa shindano la “Tusua Mapene” aliyejishindia gari jipya.

Shindano la “Tusua Mapene” liko katika msimu wake wa nne ambapo zawadi zenye thamani ya Shilingi 2.4bilioni zitatolewa kwa washindi zaidi ya 300,000. Tangu msimu wa kwanza wa shindano hili, zaidi ya Shilingi 4.8 bilioni zimeshatolewa. Kwa mara ya kwanza magari mapya manne yanakuwa mojawapo ya zawadi zinazoshindaniwa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya gari na zawadi mbalimbali kwa Washindi, Mkuu wa mauzo wa Kanda ya Kaskazini George Venanty alisema, “Leo hii, tuna mshindi aliyebahatika kujishindia gari jipya kabisa kwa kushiriki katika shindano letu la ‘Tusua Mapene’. Tumeona itakuwa vizuri ikiwa zawadi hii ya gari ikakabidhiwa wakati tukiwa tunaendeleza msimu wa upendo na kampeni yetu ya “Show Love, Tule Shangwe” kampeni yenye lengo la kurudisha tabasamu kwa wateja wa kampuni hiyo.

Kampeni ya “Show Love, Tule Shangwe” inalenga kuwapa watumiaji fursa kujishindia zawadi kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na televisheni za kisasa (Smart TV), simujanja na pesa taslimu. Zaidi ya hilo, ili kuendana na msimu wa upendo, zawadi hizi zinagawiwa pia kwa wapendwa ama wenza wa washiriki. Katika tukio hili la makabidhiano, televisheni za kisasa 6, simujanja 10 na zawadi za pesa taslimu pia zilikabidhiwa kwa washindi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai, Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini, Abbas Kayanda alisema, “Bwana Shemmy Malima Chisumo, unavyochukua gari lako, ninakuasa kutumia zawadi hii ambayo ni fursa adimu, uitumie kupiga hatua kimaisha na isiwe mwisho wa jitihada zako. Hii iwe hatua ya kwanza kwako, na uendelee kuweka bidii ili uendelee kupanda zaidi kimaisha.”

Kwa upande wake, Bwana Chisumo aliishukuru kampuni ya Vodacom, na kuwasihi wateja kushiriki shindano la Tusua Mapene, lakini pia wasambaze upendo kwa wapendwa wao ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa katika msimu huu wa Sikukuu.

Ili Kushiriki “Tusua Mapene”, mtumiaji anaweza kutuma ujumbe mfupi wenye herufi ‘V’ kwenda namba 15544 au kwa kutumia menu ya USSD kwa kupiga namba *149*01*01# na kuchagua vifurushi husika au vilevile kwa kupitia M-Pesa kwa kupiga namba *150*00# na kuchagua 3 kisha 6 na kuchagua kifurushi anachokihitaji.

Ili kushiriki na kusambaza upendo wa “Show Love, Tule Shangwe”, mteja atapiga *149*01# au atatumia App ya M-Pesa, ataingiza kitu anachokipenda huku akiambatisha na namba za simu za ndugu, jamaa au marafiki anaotaka kugawana nao zawadi iawpo atashinda.

Kuhusu Vodacom Tanzania PLC

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya huduma za mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi wa data nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa watumiaji zaidi ya milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni zake ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inamilikiwa na Vodafone Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA

Kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.vodacom.co.tz

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In