ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Wateja wa Vodacom M-Pesa kuvuna gawio la Tzs 3.4 bilioni kutoka kwa miamala ya pesa kupitia simu za mkononi.

I am Krantz by I am Krantz
Jan 31, 2022
in HABARI
0
M-Pesa customers
0
SHARES
113
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More
ADVERTISEMENT

28 Januari 2022, Dar es salaam: Kampuni ya teknolojia na mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza kuwa itatoa jumla ya TZS 3.4 bilioni ikiwa ni gawio kwa wateja wake wa M-Pesa ambao wametumia huduma hiyo robo ya nne ya mwaka jana (Oktoba hadi Disemba).
Akiongea juu ya hili, Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni alisema kuwa faida italipwa kwa wateja wote, mawakala wa rejareja na washirika wengine wa biashara wa M-Pesa ambao watapokea malipo kutokana na huduma ya malipo waliyofanya kupitia simu zao za mkononi.
“Huduma yetu ya pesa kupitia simu za mkononi, M-Pesa, inaendelea kuwa hadithi ya mafanikio ya kushangaza, ikitoa thamani kubwa ya kijamii na kifedha kwa Watanzania. Tumeona ukuaji mkubwa kwenye jukwaa la M-Pesa na wateja zaidi, mawakala, wafanyabiashara na taasisi zinazofanya biashara kufikia karibu TZS bilioni 100 kila siku. Leo tunayo furaha kushiriki katika utoaji wa gawio la Shilingi 3.4 bilioni kwa wateja wetu wapatao milioni 8 kote nchini, ”alisema.
Vodacom Tanzania PLC ina zaidi ya wateja milioni 11 kwenye jukwaa lake la M-Pesa inayomiliki sehemu ya soko ya asilimia 40 kulingana na takwimu za TCRA za hivi karibuni. Hadi sasa kampuni imelipa zaidi ya shilingi bilioni 171 ikiwa ni riba iliyolipwa tangu Julai 2015 wakati BOT ilipotunga kanuni hiyo.
Mbeteni ameongeza kuwa sehemu ya faida kwa kila mteja imehesabiwa kulingana na namna mteja alivyotumia huduma ya M-Pesa pamoja na mambo mengine, kiwango cha shughuli ambazo wamezifanya kupitia M-Pesa kwa kipindi hicho.

“Tumeanza kusambaza pesa kwenye akaunti za wateja wa M-Pesa. Wateja wanaweza kutuma neno KIASI au AMOUNT kwenda 15300 kwa ujumbe mfupi ili kujua ni kiasi gani cha faida watakachopokea. Baada ya kupokea kiasi kilichotolewa, wateja wa M-Pesa wanaweza kutumia pesa hizo kulipia huduma au kufanya matumizi ya aina yeyote wanayojisikia,”aliongeza.
“Tutaendelea kuongoza katika ubunifu, kuleta Watanzania wengi katika uchumi jumuishi wa kidijitali, kuongeza idadi ya wateja wanaotumia huduma ya M-Pesa kupitia simu za mkononi na kupanua huduma zetu za biashara, tukizingatia ushirikiano wa kimkakati na kudumisha aina anuwai za huduma ambazo hufanya malipo haraka, rahisi na salama kwa wafanyabiashara na watu binafsi vile vile,” Mbeteni alihitimisha.
Kuhusu Vodacom M-Pesa Tanzania
Vodacom M-Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu inayoongoza nchini iliyoanzishwa na Vodacom Tanzania PLC mwaka 2008. Kwa sasa ni moja ya huduma chache duniani zilizopewa tuzo ya ubora ya GSMA na ina wateja zaidi ya milioni 11. Kwa kiasi kikubwa M-Pesa imechangia katika kukua kwa huduma za kifedha na shughuli za uchumi nchini. Wateja wanatuma na kuweka pesa kupitia huduma ya M-Pesa kupitia kwa mawakala zaidi ya 106,000 nchini kote. Mfumo wa M-Pesa unaunganisha mabenki, makampuni na mashirika ya Serikali katika kufanya malipo ya kidigitali.

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
January 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Dec   Feb »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In