KAMPUNI YA BETWAY YAZINDUA PROGRAMU YA MABORESHO YA VIWANJA VYA MICHEZO TANZANIA – Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 16, 2022
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

KAMPUNI YA BETWAY YAZINDUA PROGRAMU YA MABORESHO YA VIWANJA VYA MICHEZO TANZANIA

I am Krantz by I am Krantz
Feb 7, 2022
in HABARI
0
0
SHARES
106
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

May 16, 2022

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

May 16, 2022

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

May 16, 2022
Load More

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya kimataifa, Betway Tanzania imezindua rasmi programu yake ya maboresho ya viwanja vya michezo. Programu hiyo ambayo ni sehemu ya kampuni hiyo kurudisha kwa jamii inalenga kuchangia katika juhudi za maendeleo ya sekta ya michezo nchini. Katika kutekeleza azma yake ya kuendeleza sekta ya michezo nchini Tanzania, kampuni ya Betway imeahidi kufanya mambo kadhaa ikiwemo kuchangia moja kwa moja katika maboresho ya miundombinu ya michezo, kuchangia vifaa na zana muhimu za michezo na kudhamini shughuli mbalimbali za michezo.


Kupitia programu hii ya maboresho ya viwanja vya michezo, Betway imepanga kuanza na viwanja vitano vya jijini Dar es Salaam. Kiwanja cha mchezo wa mpira wa kikapu wa Sea View kilichopo Ocean Road, Ilala, Dar es Salaam ni kiwanja cha kwanza kufanyiwa maboresho. Kiwanja hicho ambacho ni moja ya viwanja vyenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania kwa ujumla kimefanyiwa maboresho makubwa yaliyohitajika kukirudisha katika hadhi ya viwanja vya mpira wa kikapu kitaifa.


Uzinduzi wa programu hiyo umeenda sambamba na bonanza la uzinduzi wa kiwanja cha michezo wa mpira wa kikapu cha Sea View ambacho ni kiwanja cha kwanza kufanyia maboresho. Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu wamejumuika kwa kushindana na kuburudika huku wakifurahia mandhari mapya ya uwanja huo.


Akizungumza na wadau walioshiriki hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanja cha Sea View iliyofanyika Februari 5, 2022 jijini Dar es Salaam, Afisa Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe ametaja maboresho yaliyofanyika katika kiwanja hicho ambacho ni sehemu ya kituo cha michezo cha Gymkhana.


“Kama sehemu ya kuimarisha miundombinu ya michezo na kuwafanya watanzania kuipenda na kufurahia michezo tumefanya maboresho makubwa ya uwanja huu ikiwemo maboresho ya majukwaa, eneo la kuchezea, magoli, na taa kwa ajili ya matumizi ya usiku. Maboresho haya yataongeza hadhi ya uwanja huu wenye historia kubwa katika mchezo wa mpira wa kikapu lakini pia utavutia wachezaji wengi wa mpira wa kikapu kufanya mazoezi na kufanya mashindano.” Alisema Masaoe.


Akifafanua kuhusu muendelezo wa program hiyo, Masaoe aliweka wazi kuwa uzinduzi wa maboresho hayo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ambayo inatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine ya Tanzania.

“Uzinduzi wa leo ni mwanzo wa utekelezaji wa awamu ya kwanza ya maboresho ya viwanja vitano katika jiji la Dar es Salaam. Maboresho hayo yamelenga viwanja ambavyo vina matumizi makubwa katika mchezo husika ili kutoa nafasi kwa wanamichezo na mamlaka kuwa na miundombinu yenye hadhi ya kuendesha shughuli za michezo. Tunawasihi wanamichezo na mamlaka za usimamizi kusimamia vyema miundombinu hii ili iweze kuleta tija inayotarajiwa kwenye michezo kwa muda mrefu.” Alisisitiza Masaoe.

Kwa upande wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Mwenze Fiston ametoa shukurani kwa kampuni ya Betway kwa kuja na programu ya maboresho ya uwanja ambayo imeifaidisha tasnia ya mchezo wa mpira wa kikapu. Fiston aliongeza kwamba wataendelea kuhirikiana na Betway na wadau wengine kukuza mchezo wa mpira wa kikapu nchini Tanzania ili kuongeza ajira kwa watanzania wengi zaidi kupitia mchezo huo.

“Ni furaha kubwa kwetu kuona Betway ambayo ni kampuni kubwa ya michezo duniani imeona na kutambua umuhimu wa mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini na kuamua kuelekeza nguvu katika kuboresha miundombinu ya michezo hiyo. Tumepokea kwa furaha sana program hii na tunaamini haitashia hapa bali itaendelea na mikoa mingine. TBF tunawaahidi kushirikiana na mamlaka nyingine kama Shirikisho la Mpira wa Kikapu jijini Dar es Salaam na Serikali katika kutunza miundombinu ambayo imeboreshwa na Betway ili iweze kusaidia michezo kwa muda mrefu zaidi”. Alisema Fiston.


Katika bonanza la uzinduzi michezo mitatu ilichezwa ikiwemo mchezo wa maveterani wa wa mpira wa kikapu wa jiji la Dar es Salaam, mchezo kati ya Dream Team na Dar City kwa upande wa wanawake huku Dar es Salaam All Stars wakichuana na Pwani All Stars kwa upande wa wanaume. Wachezaji na mashabiki wa mpira wa kikapu wameonesha furaha yao kufuatia maboresho ya uwanja huo.

Related

I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE
HABARI

WAANDISHI WA HABARI TUMIENI KALAMU ZENU KUTANGAZA FURSA NA MATARAJIO YA MIPANGO YA SERIKALI- RC KUNENGE

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E
HABARI

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO U.A.E

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU
HABARI

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA ABU DHABI FALME ZA KIARABU

by ALLY ZINGIZI
May 16, 2022
JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA
HABARI

JOSE PESEIRO KOCHA MPYA WA NIGERIA

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022
SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI
HABARI

SERIKALI YAZITAKA TAASISI KUWAJENGEA UWEZO WAKAGUZI WA NDANI

by I am Krantz
May 16, 2022
UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI
HABARI

UKRAINE YATAKA KUUNGWA MKONO NA AFRIKA KATIKA VITA NA URUSI

by SHABANI RAPWI
May 16, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

February 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28  
« Jan   Mar »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Login to your account below

Forgotten Password?

Fill the forms bellow to register

*By registering into our website, you agree to the Terms & Conditions and Privacy Policy.
All fields are required. Log In

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In