ADVERTISEMENT
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 22, 2022
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
ADVERTISEMENT
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

SHIRIKA LA IYMT LATOA MAFUNZO YA UVIKO – 19 KWA WADAU SHINYANGA

I am Krantz by I am Krantz
Feb 3, 2022
in HABARI
0
SHIRIKA LA IYMT LATOA MAFUNZO YA UVIKO – 19 KWA WADAU SHINYANGA
0
SHARES
68
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

RelatedPosts

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

May 22, 2022

19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI

May 22, 2022

MANULA AKATWA NA KIOO

May 22, 2022
Load More
Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.

Na Mwandishi wetu – Malunde 1 blog
Shirika lisilo la kiserkali linalojishughulisha na Uwezeshaji Kiuchumi na masuala ya kiafya kwa Vijana la Igniting Young Minds Tanzania (IYMT) kwa ufadhili wa Amref Tanzania limekutana na wadau mbalimbali wa kupambana na Uviko – 19 mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kujadili matokeo ya uwepo wa ugonjwa wa Uviko 19 katika jamii sanjari na kujua namna ambavyo jamii inaendelea kupambana na ugonjwa huo.

Semina hiyo maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV imefanyika leo Jumatano Februari 2,2022 katika Ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga.

Mkurugenzi wa shirika la IYMT Michael Maganga amesema lengo la semina hiyo ni kufahamu ni namna gani jamii inaendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za ugonjwa wa Uviko 19.

“Madhumuni yetu ni kufahamu ni namna gani jamii inaendelea kujikinga na kuchukua tahadhari za ugonjwa wa uviko 19 ikwemo kuvaa barakoa,kutumia vitakasa mikono, lakini pia kupata takwimu za uchanjaji chanjo kwa wananchi zipoje na jamii imepokeaje chanjo ili tujue ni namna gani tunawezaa kusaidia na kushirikiana na wadau kuhakikisha jamii wanapata taarifa sahihi dhidi ya Uviko 19”, amesema Maganga.

“Lakini pia kusaidia na kuwaandaa watu kutoka sekta mbalimbali ili kuwasaidia wanajamii wanaokutana nao kuwapatia elimu sahihi ya Uviko 19 hususani chanjo”,ameongeza.

Kwa upande wake, Mwezeshaji katika semina, hiyo Dkt. Boniphace Kisalwa kutoka hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga amesema jamii inatakiwa kupatiwa elimu zaidi juu ya uchanjaji wa chanjo za Uviko – 19 kutokana na kuenea kwa elimu isiyokuwa sahihi juu ya chanjo za Uviko- 19 kwa wanajamii hususani kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi ya UKIMWI.

“Taarifa zinakuwa ni nyingi na mapokeo ni tofauti lakini pamoja na hayo tunahamasisha saana uchanjaji kwa watu wote lakini kundi ambalo tunalitilia mkazo ni la watu wanaoishi na maambukizi ya vurusi vya UKIMWI kwani kinga zao za mwili zinakuwa zipo chini hivyo wakichanjwa inasaidia kujiwekea ulinzi hata wakipata maambukizi hawatafika katika hatua za hatari zaidi”, amesema Dkt. Kisalwa.

Naye Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga na mratibu wa shughuli za Ukimwi Salome Komba amesema mafunzo hayo yataongeza wigo wa utoaji elimu kwa jamii ili kuondoa mitazamo hasi juu ya chanjo ya Uviko- 19.

“Kwenye kutoa elimu kuna watu kazi yao ni kupotosha hivyo tunaendelea kushirikiana kuhamasisha jamii kwamba chanjo haina madhara yeyote ni salama na tunatumia wazee maarufu, viongozi wa sungusungu kwasababu kwenye jamii zetu wakiongea watu maarufu jamii inawaamini zaidi”,ameeleza Komba

Mwezeshaji katika semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT , Dkt. Boniphace Kisalwa kutoka hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga akitoa mada kuhusu UVIKO 19

Afisa Mipango wa Shirika la IYMT Cairo Kisanga akizungumza wakati wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT
Afisa Mipango wa Shirika la IYMT Cairo Kisanga akizungumza wakati wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT
Mkurugenzi wa shirika la IYMT Michael Maganga akizungumza wakati wa semina hiyo
Meneja wa Mradi wa shirika la IYMT Violet Yongo akiwa ukumbini
Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga na mratibu wa shughuli za Ukimwi Salome Komba (kulia) akiwa ukumbini.
Sehemu ya washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakiwa ukumbini
Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.
Washiriki wa semina maalumu kuhusu Uviko – 19 na HIV iliyoandaliwa na shirika la IYMT wakipiga picha ya pamoja.

Picha zote na Mpiga picha – Malunde 1 blog
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

Related Posts

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA
HABARI

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA MAWE KIMIUJIZA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI
HABARI

19 WAJERUHIWA KATIKA AJALI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
MANULA AKATWA NA KIOO
HABARI

MANULA AKATWA NA KIOO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
NAMUNGO WAPEWA ALAMA TATU, KOCHA MAKATA AFUNGIWA MIAKA MITANO
HABARI

MAKATA, NAFTARI WAOMBA RADHI

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA
HABARI

VIFO MILIONI 8 KWA UVUTAJI WA SIGARA

by Shabani Rapwi
May 22, 2022
AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO
HABARI

AMRI YATOLEWA WATANGAZAJI WANAWAKE WAFUNIKE NYUSO ZAO

by Shabani Rapwi
May 22, 2022

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

ADVERTISEMENT

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s

KONCEPT TV
ADVERTISEMENT
Mwanaharakati Mzalendo

Mwanaharakati Mzalendo ni mtandao namba moja kwa habari makini kutoka pande zote za dunia kuhusiana na Michezo, Siasa, Afya, Elimu, Mahusiano, Vituko, n.k

Wasiliana nasi kwa Email;krantzcharles@gmail.com
SIMU; 0658123310

Follow Us

February 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28  
« Jan   Mar »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In