Mkurugenzi wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni akiwaelimisha maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi. |