ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Benki ya CRDB yasaini mkataba wenye thamani ya Sh. Bilioni 182 na Proparco kuwezesha wajasiriamali nchini

I am Krantz by I am Krantz
Mar 29, 2022
in HABARI
0
Benki ya CRDB yasaini mkataba wenye thamani ya Sh. Bilioni 182 na Proparco kuwezesha wajasiriamali nchini
0
SHARES
97
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakionyesha mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo Makao Maku ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakisaini mikataba wa makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo Makao Maku ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (kulia) wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo Makao Maku ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Proparco Afrika Mashariki, Jean Bendit-Du Chalard (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Ufaransa Tanzania, Alex David Gullion (wapili kulia), Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya,Mihaela Marcu (wakwanza kushoto), na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Benki ya CRDB wakati wa hafla ya kusaini mikataba ya makubaliano ya mkopo na dhamana za mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 182 kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali nchini, katika hafla iliyofanyika leo Makao Maku ya Benki ya CRDB. Mkopo na dhama hizo zilizotolewa na Proparco zitaiwezesha zitaiwezesha Benki ya CRDB kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa sekta ya kilimo, wajasiriamali wanawake, pamoja na wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19.
 
=======   =======   ======

Benki ya CRDB imeingia makubaliano ya uwezeshaji wajasiriamali wadogo na wakati (MSMEs) wenye thamani ya  Shilingi bilioni182 na shirika la fedha la nchini Ufaransa  la Proparco.
 
Makubaliano hayo ambayo yanajumuisha mkopo na dhamana za mikopo kwa wajasiriamali, itasaidia kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na mpango wa maendeleo wa Taifa, kwa kuzingatia zaidi wajasiriamali wanawake, wajasiriamali katika sekta ya kilimo, pamoja na wajasiriamali ambao wameathirika kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO-19. 
 
Proparco, ni kampuni tanzu ya shirika la maendeleo la UfaransaAgence Française de Développement Group (AFD Group), ambalo limejikita katika kutoa ufadhili na usaidizi kwa biashara na taasisi za kifedha barani Afrika, Asia, Amerika Kusini na Mashariki ya Kati. 
 
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka na utasaidia kwa kiasi kikubwa kufufua sekta ya ujasiriamali nchini na kuchochea ukuaji wa uchumi.
 
“Nidhahiri kuwa katika kipindi cha mitatu iliyopita wajasiriamali wengi wameathirika na janga la UVIKO-19. Tunatarajia kuwa fedha pamoja na dhamana hizi tunazozipata leo, pamoja na huduma zetu bunifu kwa ajili ya wajasiriamali, zitasaidia kuwainua na kuwawezesha wajasiriamali nchini kuboresha biashara,” amesema Nsekela
 
Nsekela alisema Benki ya CRDB imesaini mikataba mitatu na Proparco ambapo mkataba wa kwanza unajumuisha Shilingi 115 bilioni ambazo zitaelekezwa kusaidia sekta ya kilimo. Fedha hizi zitatumika kuwawezesha wakulima wadogo na wakati kufanya kilimo cha kisasa na stahimilivu kwa gharama nafuu ili kuongeza uwezo wa sekta hiyo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
 
Mkataba wa pili umehusisha Dhamana ya Mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 20 kwa ajili ya uwezeshaji wa wajasiriamali walioathirika na janga la UVIKO-19. Nsekela mesema dhamana hiyo ya mikopo itawezesha kuwainua wajasiriamali wengi walioathirika na kutoa matumaini mapya katika biashara zao. Dhamana hiyo ni sehemu ya mpango wa uwezeshaji unaotekelezwa na Serikali ya Ufaransa kupitia program ya ‘Choose Africa’ inayotekelezwa na AFD.
 
Mkataba wa tatu umehusisha Dhamana ya Mikopo ya EURIZyenye thamani ya Shilingi bilioni 47 kwa ajili ya uwezeshaji wa wajasiriamali wanawake nchini. Dhamana hiyo inaambatana na mafunzo kwa wajasiriamali wanawake ili kusaidia kuboresha biashara zao. Dhama hiyo ya Mikopo ya Euriz inawezeshwa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF), Jumuiya ya Nchi za Carribean na Pacific (OCPAZ).
 
Katika maelezo yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Proparco, Gregory Clemente alibainisha kuwa fedha na dhamana hizo zilizotolewa zitachangia kwa kiasi kikubwa malengo ya programu ya Chagua Afrika, mpango wa uwezeshaji wajasiriamali Afrika unaotekelezwa na Serikali ya Ufaransa uliozinduliwa mwaka wa 2018. 
 
“Proparco inafuraha kuanzisha uhusiano huu na Benki ya CRDB na kuikaribisha kama mshirika mpya wa mpango wa Chagua Afrika. Hatua hii ya kusaini mikataba inaonyesha dhamira ya Proparco kwa wajasiriamali wa Tanzania, na ni matumaini yetu ushirikiano huu utaiongezea uwezo Benki ya CRDB katika uwezeshaji wajasiriamali kupitia mikopo nafuu,” alisema Clemente.
 
Benki ya CRDB inaongoza katika juhudi za kusaidia wajasiriamali nchini Tanzania kupitia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na benki hiyo. Kupatikana kwa fedha na dhamana hizo kutaisaidia Benki ya CRDB kuongeza uwezo wake katika kuwawezesha wajasiriamali nchini jamba ambalo litasaidia kuchochea ukuaji endelevu, kukuza ajira, ujuzi na uzalishaji mali nchini.

—

RelatedPosts

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AIPONGEZA BENKI YA CRDB, AHITIMISHA MAONESHO YA NANENANE JIJINI MBEYA

Aug 9, 2022

BENKI YA CRDB YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE KITAIFA, JIJINI MBEYA

Aug 2, 2022

WAZIRI MBARAWA AWATAKA WAKANDARASI NA WAZABUNI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEZESHAJI KUTOKA BENKI YA CRDB

Jul 21, 2022
Load More
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: CRDB
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In