Mwimbaji wa Bongofleva, Zuchu amefunguka ya moyoni kwa yale ambayo anaona hayapo sawa kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania.
Zuchu amesema bado haki za wasanii zinachezewa lakini bado kuna watu wanafanya mzaha na kuwatumia wasanii kama daraja la kupata umaarufu. Kupitia Insta Story Zuchu ameandika;
Ni Tanzania pekee ndoa tuna industry ya muziki iliyojaa mzaha na vichekesho ndani yake. Inatia aibu maana hii mtandao tunaitumia kujichoresha kwa michezo ya kitoto tunayoicheza.
Mimi niwashukuru Watazania mlio wengi bila hata kushurutishwa mnajua mbivu na mbichi, mnatupambania sana wasanii wenu thats the only thing kinanipa nguvu sababu nyie ndo mnatuweka tulipo. But as for the industry yetu kwa ujumla inatia huruma na hasira.
Imagine hata sehemu ya kufanya show za maana hatuna, haki zetu ndio hizo zinachezewa sandakalawe, tunafanywa daraja la watu wasiojali tasnia kupata umaarufu tu wa kupatia vipato.
cc @officialzuchu