Katika chapisho fupi kwa Instagram, mwigizaji huyo aliandika juu ya “msimu wa uponyaji” akimaanisha tukio la Oscars.
Mume wake, Will Smith, alilaaniwa na waandaji wa tuzo hizo kwa kumzaka kofi Rock.
Aliomba msamaha siku ya Jumatatu, akitaja tukio hilo kuwa vurugu “sumu na uharibifu”.
Tukio hilo la Jumapili usiku lilitokea kabla tu ya Smith kushinda tuzo ya Oscar ya Muigizaji Bora, wakati mchekeshaji Rock alipokuwa jukwaani kutoa tuzo ya Makala Bora.
Alifanya mzaha kuhusu kichwa kilichonyolewa cha Pinkett Smith, iliyotokana na ya hali ya upotezaji wa nywele alopecia.
Pinkett Smith hakutoa maoni yake huku kukiwa na mzozo mkali na mjadala wa hadharani uliofuata kuhusu utani wa Rock na vitendo vya Smith hadi Jumanne, akichapisha kwenye Instagram: “Huu ni msimu wa uponyaji na niko hapa kwa ajili yake”.
Rock bado hajatoa maoni yake hadharani juu ya kile kilichotokea kwenye tuzo za Oscar au msamaha wa Smith.
Hata hivyo, tikiti za maonyesho yake yajayo ya vichekesho zimeripotiwa kupanda kufuatia tukio la Jumapili.