Jenerali wa Urusi Luteni Jenerali Yakov Rezantsev, ambaye inasemekana alifariki Jumamosi, ndiye afisa wa cheo cha juu zaidi kuuawa, kulingana na wizara ya ulinzi ya Ukraine.
Wataalamu wanasema ari ya chini kati ya wanajeshi wa Urusi imewalazimu maafisa wakuu kuwa mstari wa mbele.
Mwandishi wetu wa masuala ya usalama Frank Gardner anasema vifo vilivyoripotiwa huenda vilitokana na majenerali kulazimika kuwa mbele katika mapigano ili kuwaondoa wanajeshi wao kutokana na kuzomewa.
Mafumo wa kijeshi ya Kirusi huwa unasubiri amri kutoka juu.
Afisa mstaafu wa Jeshi la Uingereza alisema vifo vya majenerali hao pia kumeonesha “mafanikio ya kiwango cha juu ambao unaweza kudhalilisha mfumo wa kijeshi wa Urusi”.