Kinara wa mabao Ligi Kuu ya NBC, Fiston Mayele, Raia wa Congo DR anayekipiga kunako Mtaa wa Jangwani amesema ataendelea kutetema na Wananchi (Mashabiki wa Timu yake ya Yanga) kwani wamekuwa wakimpa sapoti kubwa na kuipa sapoti timu kila mechi.
Mayele amesema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wa Yanga dhidi ya KMC ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 2-0 huku Mayele akishindilia bao la kwanza na kufikisha mabao 11 mpaka sasa katika Ligi hiyo hivyo kumfanya kuwa kinara wa mabao huku Yanga wakiendelea kujikita kileleni kwa kuwa na pointi 48 mbele ya Simba wenye pointi 35.
“Mechi ilikuwa ngumu kipindi chakwanza kwasababu safu ya ulinzi haikuanza vizuri baada ya Kupata bao la kuongoza timu ilitulia tukaanza kutafuta bao la pili.
Kuhusu Mimi kufunga Kila wakati sili ipo kwenye mazoezi ninayofanya na mashabiki wangu wengi wanapenda kutetema na Mimi,nawapenda sana mashabiki wa klabu ya Yanga ntaendelea kutetema nao,” amesema Mayele.