Mwenyekiti wa chama cha T.L.P Augustino Mrema ametangaza rasmi kufunga ndoa nyingine, Alhamisi ya Machi 24 katika Parokia ya Uwomboni Mkoani Kilimanjaro.
Mrema mwenye umri wa miaka 77 amesema amepata binti mweupe na mwenye umri mdogo ambaye ndiyo chaguo lake kwasasa na hana budi kufunga nae pingu za maisha.
Ndoa hii ya Mrema inakuja mara baada ya kumpoteza aliyekuwa Mke wake Bi.Rose Mrema ambaye alifariki mwaka jana.