Mtoto mwenye nguvu kiutawala wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameelezea kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Jenerali Kainerugaba – ambaye ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda – aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, kwamba ” “binadamu wengi (ambao si wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine”.
“Putin yuko sahihi kabisa!” aliongeza.
“Wakati USSR ilipoweka makombora yenye silaha za nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, nchi za Magharibi zilikuwa tayari kulipua ulimwengu juu yake. Sasa Nato ikifanya hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti.”
Jenerali Kainerugaba ndiye afisa mkuu wa kwanza wa kijeshi barani Afrika kuunga mkono hadharani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Anasemekana kuwa anaweza kuwa mrithi wa babake mwenye umri wa miaka 77, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.
Umoja wa kanda ya Afrika Magharibi Ecowas umelaani uvamizi wa Urusi, huku Umoja wa Afrika ukiitaka Moscow kuheshimu “eneo la uadilifu.
Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imetoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Urusi kutoka Ukraine.
Jenerali Kainerugaba pia alimtuma tena ujumbe wa mwanahabari mashuhuri wa Uganda Andrew Mwenda, ambaye alisema kwamba hata “mgeni katika siasa za kimataifa anaweza kuona kwamba Moscow haiwezi kamwe kuruhusu Ukraine kujitosa kwa Nato, EU, kwa sababu inaleta tishio kwa Urusi!