ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Naibu Spika aipongeza Benki ya NMB kwa kuwakumbuka Wamachinga

I am Krantz by I am Krantz
Mar 16, 2022
in BIASHARA
0
Naibu Spika aipongeza Benki ya NMB kwa kuwakumbuka Wamachinga
0
SHARES
113
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Hassan Zungu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala jijini Dar es Salaam, ameishukuru Benki ya NMB kwa kulikumbuka kundi la wafanyabishara ndogo ndogo nchini maarufu Wamachinga na kuwasaidia kukua.

RelatedPosts

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

MESUT ÖZIL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA

Mar 23, 2023

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Mar 23, 2023

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

Mar 23, 2023
Load More

Benki ya NMB ilimkabidhi Naibu Spika laptop 5 zenye thamani ya Tsh. Milioni 7.5 kusaidia upatikanaji wa database wa kundi hilo.

Baada ya kupokea vifaa hivyo, Mh. Mussa Hassan Zungu alivikabidhi kwa viongozi wa SHIUMA, tawi la Ilala kwa ajili ya matumizi ya kiofisi ikiwemo kuweka Kanzi Data(database), ili iwe rahisi kutambulika na kujua shughuli wanazofanya popote walipo nchini.

ADVERTISEMENT

Zungu ameisifu NMB kuwa ni benki ya kipekee iliyoonyesha kwa vitendo kujali maisha ya wafanyabiashara wadogo, kwa kuwasaidia mitaji na kuangalia ukuaji wao.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi NMB, Filbert Mponzi alisema vifaa hivyo ni mwendelezo wa makubaliano waliyoingia kati yao na SHIUMA, lengo ni kutengeneza Kanzi Data itakayowasaidia kujulikana kirahisi na kufikika.
Pia, angependea kuona Wamachinga wamesajiliwa, wawe rahisi kufikika.

Alibainisha kuwa pamoja na makabidhiano ya vifaa hivyo, NMB imeendelea kushirikiana na kundi hilo la wafanyabiashara wadogo tangu mwaka 2000. Kwa wastani, benki ya NMB hutoa mikopo ya thamani ya Sh Bil 50 kila mwezi kwa kundi hilo la wafanyabishara wadogo wakiwemo Wamachinga.

Kwa upande wake Katibu wa Wamachinga Kariakoo, Thabit Maloka aliyemwakilisha Mwenyekiti wa SHIUMA Taifa, alisema wamepata faraja kubwa kwa msaada huo kutoka NMB, wanaamini hayo ni matunda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na ahadi aliyowapa kuwashika mkono.

Alibainisha kuwa wanaamini huo ni mwanzo tu, kwani wanajua mazuri yanakuja. Ambapo aliuomba uongozi wa NMB kufikiria kuongeza msaada zaidi ikiwemo kufanya ukarabati wa majeng ya ofisi zao za Ilala jijini Dar es Salaam pamoja na kuwapa mafunzo ya ujasiriamali.
Kompyuta hizo tano zinakwenda kujenga mifumo ya mawasiliano, ufuatiliaji na tathmini katika shughuli za Wamachinga pamojaa na kuwasaidia Wamachinga kuwa na mfumo mzuri wa kufanya biashara zao.

ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

TCB YATOA MSAADA WA MABATI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI BUTIAMA
BIASHARA

TCB YATOA MSAADA WA MABATI KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI BUTIAMA

by Ally Hamis Zingizi
Mar 22, 2023
MPYA: TigoPesa yazindua Kadi Mtandao (Tigo Pesa Mastercard)
BIASHARA

MPYA: TigoPesa yazindua Kadi Mtandao (Tigo Pesa Mastercard)

by ALFRED MTEWELE
Mar 22, 2023
BRELA YAWATAKA VIJANA KUSAJILI BIASHARA ZAO
BIASHARA

BRELA YAWATAKA VIJANA KUSAJILI BIASHARA ZAO

by ALFRED MTEWELE
Mar 14, 2023
USINUNUE GESI KWA WASIO NA MIZANI
BIASHARA

USINUNUE GESI KWA WASIO NA MIZANI

by ALFRED MTEWELE
Mar 9, 2023
BENKI YA AKIBA WAZINDUA WARIDI AKAUNTI   KWA  WANAWAKE WAJASIRIAMALI
BIASHARA

BENKI YA AKIBA WAZINDUA WARIDI AKAUNTI KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

by I am Krantz
Mar 9, 2023
NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda
BIASHARA

NMB yafadhili ziara ya mafunzo Machinga, Bodaboda Dar nchini Rwanda

by I am Krantz
Feb 3, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In