ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Saturday, April 1, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

NMB, eGovernment Z’bar zasaini makubaliano Makusanyo Mapato

I am Krantz by I am Krantz
Mar 16, 2022
in HABARI
0
NMB, eGovernment Z’bar zasaini makubaliano Makusanyo Mapato
0
SHARES
107
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter



RelatedPosts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

Apr 1, 2023

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

Apr 1, 2023

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

Apr 1, 2023
Load More


Benki ya NMB na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kupitia Wakala wa Serikali Mtandao ‘eGovernment Zanzibar’, wamesaini makubaliano ya ushirikiano, yatakayowezesha mifumo ya NMB kuingiliana na ile ya ZanMalipo, hivyo kuwezesha taasisi za SMZ, kukusanya mapato kupitia matawi na mifumo ya kidijitali ya benki hiyo.

Makubaliano hayo yamefanyika leo visiwani Zanzibar, ambapo Benki ya NMB imeimarisha ushirikiano huo ambao utakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi visiwani humo, na kwamba inaamini utakuwa wa karibu zaidi, endelevu na wenye manufaa kwa SMZ na taasisi zake lakini pia utakaoleta maendeleo chanya.


Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, aliipongeza SMZ chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa mageuzi chanya ya kiuchumi yanayochakatwa na kusimamiwa na serikali yake kwa ustawi wa Taifa.


Zaipuna alibainisha kuwa makubaliano hayo ni chachu kwa taasisi yake kubuni suluhushi mbalimbali za Wazanzibar na Taifa ujumla, na kwamba maendeleo ya kidijitali kwa ulimwengu wa sasa hayaepukiki, hivyo ushirikiano wao huo utakuwa na mchango chanya katika kuharakisha ukuzaji uchumi na kurahisisha utendaji wa Serikali.

ADVERTISEMENT


Makubaliano haya ni kielelezo tosha kuwa Serikali ya Zanzibar na NMB itashirikiana kuboresha huduma za ukusanyaji mapato na malipo, sambamba na kuwezesha mifumo yetu kuingiliana na ile ya ZanMalipo, hivyo kuwezesha Taasisi za SMZ kukusanya mapato kupitia matawi ya NMB na mifumo ya kidijitali ya Benki hio.

Kupitia makubaliano haya, NMB na eGovenment Zanzibar, tunaenda kutengenezea Kituo cha Pamoja cha Malipo Kidijitali ‘One Stop Center,’ cha Shirika la Bandari Zanzibar, ambacho kitampa mlipaji wa huduma mbalimbali ‘control number’ moja kwa ajili ya kufanyia malipo mbalimbili bandarini, badala ya namba tofauti tofauti.


Suluhisho hizi mbili zinazooambatana na makubaliano haya, zinaenda kuboresha utoaji huduma kwa wananchi, lakini pia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato na kuondoa kero ya muda mrefu wanaotumia wananchi kufanya huduma za malipo.

ADVERTISEMENT


Alibainisha kuwa, SMZ kupitia eGovenment na NMB, wanaenda kujenga ushirikiano utakaokuwa chachu ya ukuaji wa uchumi na kwamba matarajio yao ni kuwa na ushirikiano endelevu, wa karibu zaidi, wenye manufaa kwa SMZ na taasisi zake, utakaoleta maendeleo chanya ya Serikali, Taifa na wananchi kwa ujumla.


Mkurugenzi Mtendaji wa eGovernment Zanzibar, Said Seif Said, aliishukuru NMB kwa kusaini makubaliano ya ushirikiano huo, ambao aliutaja kama muarobaini wa changamoto mbalimbali za kimalipo wanazokutana nazo wananchi wa Zanzibar, unaoenda pia kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali.


Seif alisema eGovernment tunaamini kwamba ushirikiano huu ni chanya, utakaobeba tija kwa Serikali, hususani hiyo ‘One Stop Center’ ambayo itajikita katika kurahisisha mifumo ya malipo bandarini ambako tutatumia mifumo ya kidijitali kuongeza ufanisi  kwenye makusanyo mbalimbali.

Pia, huu utakuwa ni mwanzo tu, tunategemea kufanya mengi makubwa kwa pamoja baina yetu na NMB. Bandarini ni sehemu ambako kumekuwa na changamoto za muda mrefu katika masuala mazima ya makusanyo, lakini kupitia makubaliano haya tunaamini yataondoa na kumaliza changamoto zote hizo.

Related

I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI
HABARI

YANGA TUNAHITAJI KUIFUNGA MAZEMBE TUONGOZE KUNDI

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA
HABARI

GARI LA KIFAHARI ZAIDI NA LENYE THAMANI KUBWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA
HABARI

ONYANGO AOMBEWA MSAMAHA KWA ALICHOFANYA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA
HABARI

KOCHA NABI NA WACHEZAJI HAWA KUKOSA MCHEZO DHIDI YA MAZEMBE, SABABU YATAJWA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022
HABARI

TANI 20.6 ZA BANGI ZIMEKAMATWA 2022

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023
SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA
HABARI

SAFU YA ULINZI IMEWAANGUSHA SIMBA

by Shabani Rapwi
Apr 1, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In