ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

Pigo kwa Rais Putin mshauri wake akijiuzulu na kutoroka Urusi

I am Krantz by I am Krantz
Mar 24, 2022
in HABARI
0
Pigo kwa Rais Putin mshauri wake akijiuzulu na kutoroka Urusi
0
SHARES
132
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

Anatoly Chubais amejiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa na kutoroka Urusi

Duru ilidokeza kuwa Chubais alijizulu na kuondoka Urusi kutokana na vita vya Ukraine

RelatedPosts

Rais wa Marekani: Putin hawezi kubaki madarakani

Rais wa Marekani: Putin hawezi kubaki madarakani

Mar 27, 2022
Load More

Kujiuzulu kwake ni baada ya Rais Putin kuonya kwamba ataisafisha Urusi dhidi ya “uchafu na wasaliti” anaowatuhumu kufanya kazi kisiri na Marekani

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepata pigo kubwa baada ya mmoja wa washauri wake, Anatoly Chubais kujiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa.

Pigo Kubwa kwa Rais Putin Baada ya Mshauri wake Kujizulu na Kutoroka Urusi

Anatoly Chubais kujiuzulu kutoka jukumu lake kama mjumbe wa kimataifa. Picha: Andrey Rudakov/Bloomberg.

ADVERTISEMENT

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini Urusi, Chubais kwa sasa yuko Uturuki na mke wake.

Chubais, 66, ambaye ni mwanamageuzi mkongwe wa Urusi, alipewa kazi ya kuratibu malengo ya maendeleo endelevu ya taifa hilo kimataifa.

Kujiuzulu kwake kunakujia baada ya kuchapisha picha ya kiongozi wa upinzani wa Urusi, Boris Nemtsov aliyeuawa mnamo Februari 2015, katika kile kilichoonekana kama ishara mbaya wakati vita vya Urusi na Ukraine vilipoanza.

Hata hivyo, hakuambtanisha ujumbe wowote katika kumbukumbu ya kuuawa kwake Nemtsov akionyesha kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Natazamia Kuona Tiketi ya Ruto – Karua Itakayookoa Taifa la Kenya: Moses Kuria

Japo hajatoa taarifa yoyote kuhusu kujiuzulu kwake, duru ilidokezea shirika la habari la Reuters kuwa Chubais alijizulu na kuondoka Urusi kutokana na vita vya Ukraine.

Akijulikana kama mbunifu wa ubinafsishaji wa Urusi wa miaka ya 1990, Chubais alimpa Putin kazi yake ya kwanza Kremlin katikati ya miaka ya 1990, na aliunga mkono kupanda kwake mamlakani mwishoni mwa muongo huo.

ADVERTISEMENT

Chini ya Putin, Chubais alichukua nyadhifa za juu katika makampuni makubwa ya serikali hadi rais huyo alipomteua mjumbe maalum mwaka 2021.

Kujiuzulu kwake pia kunakujia baada ya Rais Putin kuonya mnamo Machi 16, 2022, kwamba ataisafisha Urusi dhidi ya “uchafu na wasaliti” anaowatuhumu kufanya kazi kwa siri na Marekani.

“Watu wowote, na haswa watu wa Urusi, wataweza kila wakati kutofautisha wazalendo kutoka kwa takataka na wasaliti na kuwachomoa kama kisu aliyeruka vinywani mwao kwa bahati mbaya.”

“Nina hakika kwamba utakaso huu wa asili na muhimu wa jamii utaimarisha tu nchi yetu, mshikamano wetu, mshikamano na utayari wa kukabiliana na changamoto yoyote,” Rais Putin alisema.

Ngilu Ataka DP Ruto Kukoma Kujipiga Kifua Kisa Kumsaidia Uhuru Kupata Urais: “Ni Uhuru Alikupa Ajira”

Wiki iliyopita, Arkady Dvorkovich, ambaye alikuwa mshauri mkuu wa uchumi wa Dmitry Medvedev wakati wa urais wake na naibu waziri mkuu hadi 2018, alijiuzulu kama mkuu wa hazina ya teknolojia ya Skolkovo inayoungwa mkono na serikali baada ya kulaani uvamizi huo.

Dvorkovich, ambaye pia ni rais wa Shirikisho la Kimataifa la Chess, ni mmoja wa maafisa wachache waandamizi wa zamani waliozungumza dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Related

Tags: PUTIN
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA
HABARI

WABUNGE WAONYA KUWEKEA VIKWAZO SHERIA YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA
HABARI

UWANJA WA NDEGE CHATO KUBORESHWA

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI
HABARI

ASHTAKIWA MAHAKAMANI KUWAINGILIA MBUZI KIMWILI

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati
HABARI

NMB yatoa msaada wa milioni 39 kuimarisha sekta ya afya na elimu Kanda ya Kati

by I am Krantz
Mar 23, 2023
Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Jumatatu Februari 6,2023
HABARI

Yaliojili Kwenye Kurasa za Magazeti ya Leo Alhamisi Machi 23,2023

by ALFRED MTEWELE
Mar 23, 2023
YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE
HABARI

YANGA PRINCESS, SIMBA QUEENS HAKUNA MBABE

by Shabani Rapwi
Mar 22, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In