ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Monday, March 20, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

RAIS SAMIA APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WENYE MAHITAJI MAALUM KUTOKA NMB

I am Krantz by I am Krantz
Mar 9, 2022
in HABARI
0
RAIS SAMIA APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WENYE MAHITAJI MAALUM KUTOKA NMB
0
SHARES
110
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (kushoto) akipokea Vifaa vya kusaidia kusikia kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Uhuru Mchanganyiko, Jangwani, na Shule ya Msingi Uhuru Wasichana, wakati wa ziara ya Rais kutembelea shule hiyo katika hafla maalumu ya Uboreshaji Elimu kwa kuzingatia mahitaji maalum. Katika hafla hiyo Benki ya NMB ilikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh. milioni 58. 


RelatedPosts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

Mar 20, 2023

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

Mar 20, 2023

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

Mar 20, 2023
Load More

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (kushoto) akipokea Vifaa vya michezo na Jezi kutoka kwa Ofisa Mtendaji mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, ikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, wakati wa ziara ya Rais kutembelea shule hiyo katika hafla maalumu ya Uboreshaji Elimu kwa kuzingatia mahitaji maalum. Katika hafla hiyo Benki ya NMB ilikabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Tsh. milioni 58. 

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kwa mchango unaoenda kufanikisha uboreshaji elimu kwa makundi maalum, ambako imetoa msaada wenye thamani ya Sh. Mil. 58, wa vifaa mbalimbali, vikiwemo vya kusaidia kuona na kusikia kwa shule 4 jijini Dar es Salaam.

Rais Samia alitoa poongezi hizo wakati wa ziara maalum katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Kariakoo, iliyolenga kufanikisha maboresho mbalimbali ya elimu wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule za sekondari Benjamin Mkapa, Uhuru Mchanganyiko na Jangwani, na Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.

Katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu NMB, Ruth Zaipuna, aliyemkabidhi Rais Samia vifaa maalum 60 vya kusaidia wanafunzi wenye uziwi, vifaa 90 vya kusaidia wenye ulemavu wa macho – vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 24, pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’ 20 zenye thamani ya Sh. Mil. 20 na vifaa vya michezo vya Mil. 14.

 “Serikali imetumia Sh. Bil. 5.9 katika uboreshaji elimu ngazi ya awali, msingi, sekondari na vyuo, ili kuhakikisha wenye mahitaji wote wanapata elimu nchini. Nawashukuru sana NMB kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu Ruth Zaipuna, kwa kubeba changamoto za vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hizi.

 “CEO wa NMB hapa amenikabidhi vifaa vya kusaidia usikivu, uoni na hata kompyuta mpakato 20, ombi langu kwenu ni kutuongezea ‘laptop’ kama hizo kwa sababu shule hizi ni nyingi na mahitaji ya hizo kompyuta ni mengi. Tunawaomba mtusaidie katika hili ili kupunguza changamoto hiyo kwa vijana wetu,” alisisitiza.

 

Akizungumza wakati akimkabidhi msaada huo, CEO wa NMB, Zaipuna alisema: “Mheshimiwa Rais, NMB ni mdau mkubwa wa elimu Tanzania, ndio maana tumekuja hapa kukuunga mkono katika jitihada za Serikali yako za kuhakikisha Watanzania wanapata elimu bora. 

ADVERTISEMENT

 

“Tumekuja hapa na vifaa vya kusaidia kuona 90, vya kusaidia kusikia 60, ‘laptop’ 20, pamoja na vifaa vya michezo katika shule hizi.

 

“Misaada hii inayolenga kusaidia wanafunzi wa shule hizi, tunaamini itaenda kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zilizoelezwa katika risala ya shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa, huku vifaa vya michezo tukiamini vitasaidia kuboresha michezo kwa ustawi wa afya za wanafunzi wetu katika shule husika,” alisema Zaipuna.

ADVERTISEMENT

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, aliitaja NMB kama ‘mkono wa kulia wa Serikali ya mkoa’ wake, kwa namna inavyojitoa kupambana na maboresho kwenye Sekta ya Elimu na miundombinu yake, lengo likiwa kuunga mkono jitihada za kufanikisha elimu bora kwa wanafunzi wa mkoa wake.

 

*****Mwisho*****

 

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

RJ THE DJ VIFO VINAONGEZA MSONGO WA MAWAZO
HABARI

ROMY JONS AOMBA MSAMAHA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”
HABARI

MCHUNGAJI AFUNGA KANISA KISA ASHINDA MIL 100 ZA “KUBETI”

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA
HABARI

WAZIRI BITEKO ATAKA BAJETI YA 2023/24 KUZINGATIA VIPAUMBELE VYA WIZARA

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO
HABARI

TMA YATOA TAHADHARI MVUA KUBWA MIKOA HII KUANZIA LEO NA KESHO

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023
WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR
HABARI

WATU 5 WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA WIZI MAFUTA SGR

by ALFRED MTEWELE
Mar 20, 2023
MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI
HABARI

MARUFUKU KUTOA FEDHA UPATE DHAMANA POLISI

by Shabani Rapwi
Mar 20, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In