Rais wa Tunisia, Kais Saied ameonya kuhusu majaribio ya kufanya vikao vya bunge ambalo limesimamishwa.
Akizungumza jana usiku Saied amesema vikosi na tasisi vitaendelea kupambana na wale wanaojaribu kuwasukuma Watunisia kupigana.
Mapema jana, Spika wa Bunge la Tunisia, Rached Ghannouchi alisema kwamba bunge hilo litafanya vikao vyake kamili viwili wiki hii, kujaribu kubatilisha hatua za Rais Saied kuelekea katiba mpya na kujilimbikizia madaraka ambao ni sawa na utawala wa mtu mmoja.
Julai mwaka uliopita, Rais Saied alilivunja bunge hilo na kuimarisha mamlaka yake kamili, hatua ambayo wapinzani wameielezea kama mapinduzi. Kiongozi huyo wa Tunisia amesema nchi hiyo sio kibaraka na kwamba majaribio hayo yanakatisha tamaa, hayafuati sheria na hayana manufaa kwa taifa hilo.