Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Steve Nyerere amemuomba Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa kuangalia upya mchakato wa Tuzo za Muziki Tanzania baada ya kutangaza majina ya wanaowania.
Pia Steve Nyerere amesema anaamini Waziri Mchengerwa atatumia busara zake katika jambo liloibua mjadala mara baada ya wasanii wa WCB Wasafi kukosekana. Kupitia Insta Steve Nyerere ameandika;
Leo hii wapo Watanzania wanataka kuona Zuchu kashindanishwa na nani, leo hii Watanzania wanataka kuona Mbosso yupo kundi gani, Rayvanny yupo kwenye kategori ipi lakini hili mnataka kulifumbia macho kwa jeuri tu haiwezekani.
Tuzo ndio sehemu pekee ambayo haina makundi kuna muziki mzuri sio matimu fulani, no hapa ni muziki tu, na tunaposema tuzo za ndani hakuna mtu atazipinga maana heshima huanzia nyumbani kwako kwanza.
Naimani sana na Mhe. Mchengelwa kwa hili, naimani naye kubwa atatumia busara kukaa kitako na WCB Wasafi pamoja na uongozi mzima kwa faida ya mashabiki wa muziki wetu.
Kama kweli tunania ya kuboresha sanaa yetu basi hakuna haja ya kuvutana kuna haja ya kukaa chini na kukubaliana na wasanii wote kuwa tunaenda kujenga nyumba moja haina haja ya kugombea fito.
Niombee Wizara yetu pendwa tuangalie mchakato huu upya kabisa kwa maslahi ya kuinua na kupeleka mbali zaidi muziki wetu.
cc @stevenyerere2 @wcb_wasafi