ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Friday, March 24, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

TMA yatoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa mwaka 2021

I am Krantz by I am Krantz
Mar 3, 2022
in HABARI
0
TMA yatoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya Klimatolojia ilivyokuwa mwaka 2021
0
SHARES
120
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya  Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya  Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo kwa waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang’a.

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa rasmi ya Mwenendo wa Hali ya  Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021, huku ikiainisha ulikuwa na hali mbaya ya kiujumla iliyoambatana na madhara kwa baadhi ya maeneo.

 Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari leo jijini dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi alisema kwa mwaka 2021 Tanzania ilikumbwa na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko na upungufu wa mvua pia katika baadhi ya maeneo, joto pamoja na upepo mkali.

“…Itakumbukwa kuwa mwaka wa 2021, nchi yetu ilikumbwa na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa zilizoambatana na mafurikona upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo, joto pamoja na upepo mkali.  Maeneo yaliyoathiliwa na mafuriko ni pamoja na mikoa ya kusini na magharibi mwa nchi ambapo yalisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja, makazi, na mashamba,” alisema Dkt. Kijazi.

Alitolea mfano, kuwa tarehe 12 Januari 2021 Mvua kubwa ya milimita 369.7 ilinyesha Mtwara na kuvunja rekodi ya mvua iliyowahi kupimwa ndani ya saa 24 katika Kituo cha Hali ya Hewa cha Mtwara tangu kuanzishwa kwake mwaka 1951. Pia, mvua ya mawe iliyoleta taharuki ilinyesha wilayani Biharamulo tarehe 14 Agosti 2021, kipindi ambacho kawaida huwa hakina mvua kwa maeneo hayo.

Hata hivyo, aliongeza kuwa kipindi cha ukavu cha muda mrefu kilitokea katika miezi ya Oktoba na Disemba 2021 na kusababisha athari kubwa kwa jamii na uchumi hasa jamii za wafugaji ambapo idadi kubwa ya mifugo ilikufa kwa njaa na kukosa maji katika baadhi ya maeneo ya mikoaya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Manyara na Pwani. 

“…Kutokana na changamoto hizi za hali ya hewa ambazo zimekuwa zikijirudia mara kwa mara, Mamlaka imejikita kufanya uchambuzi wa kina wa hali ya hewa kila mwaka na kisha kutoa ripoti ya hali ya Klimatolojia kwa mwaka husika,” alisisitiza Dkt. Kijazi ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO). 

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya  Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo kwa waandishi wa habari, kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang’a.


RelatedPosts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

Mar 24, 2023

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

Mar 24, 2023

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

Mar 24, 2023
Load More
ADVERTISEMENT
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa, Dk. Ladislaus Chang’a akifanya wasilisho kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.


Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akisisitiza jambo alipokuwa akitoa taarifa ya Mwenendo wa Hali ya  Klimatolojia ilivyokuwa kwa mwaka 2021 leo jijini Dar es Salaam.
Aidha, ripoti hiyo inatoa taarifa za kina kuhusu matukio ya hali mbaya ya hewa yaliyotokea na madhara yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia hubainisha ukubwa wa matukio haya kwa kulinganisha na matukio ya namna hiyo yaliyotokea miaka iliyopita. Mwaka 2021 ulikuwanajotojuuyawastaniwamudamrefu (1981-2010) kwa kiwango cha nyuzijoto0 50C. Hali kama hiyo inaweza ikawa imeathiri afya ya binadamu na wanyama, uzalishaji, usindikaji na uhifadhi wa vyakula.

“Sambamba na Taarifa hii ya Klimatolojia, napenda nitumie fursa hii tena kukumbusha hususan wataalam katika sekta mbalimbali kufuatilia taarifa mpya ya tathmini ya mabadiliko ya hali ya hewa kuhusiana naA thari na Uhimilivu wa mabadiliko ya hali ya hewa iliyotolewa la tarehe 28 Februari 2022 na Jopo la Kiserikali la Tathmini ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC).”
ADVERTISEMENT

Related

ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE
HABARI

BABA MWENYE NYUMBA AFUMANIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA
HABARI

WANAOKULA HADHARANI MCHANA WA RAMADHANI KUKAMATWA

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII
HABARI

HII KALI : KUISHI CHINI YA MAJI SIKU 100 KISA KUTAFUTA REKODI HII

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI
HABARI

WANAUME WANAONYANYUA VITU VIZITO WATAJWA RIJALI ZAIDI

by Shabani Rapwi
Mar 24, 2023
MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI
HABARI

MWALIMU JELA MIAKA 30 KWA KUMLAWITI MWANAFUNZI

by ALFRED MTEWELE
Mar 24, 2023
BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC
HABARI

BENKI YA NBC YAZINDUA KAMPENI YA MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC

by I am Krantz
Mar 24, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In