Mshauri mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameambia kipindi cha BBC Radio 4’s World at One kwamba Ukraine “haiko tayari kuacha eneo lolote”.
Akizungumza katika mkesha wa mazungumzo zaidi kati ya Urusi na Ukraine, Alexander Rodnyansky alisema “sasa shinikizo ni kwa Urusi”.
“Ni wazi, hawawezi kuendeleza vita hivi kwa miaka mingi na ari yao iko chini sana hata hawawezi kuendelea kuviopa vikosi vyao vifaa kuendelea na mapigano,” alisema.
Bw Rodnyansky, ambaye pia ni profesa msaidizi wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Cambridge, alisema Ukraine haitasilimisha “uadilifu wa kieneo”.
Quote Message: Ukiwauliza watu wanaoishi katika maeneo haya, hawataki kuishi Urusi. Je, tunawezaje kuwaacha? Achilia mbali wazo zima la kuikata nchi yetu from Alexander Rodnyansky Mshauri Mkuu wa Volodymyr Zelensky wa Ukraine
Ukiwauliza watu wanaoishi katika maeneo haya, hawataki kuishi Urusi. Je, tunawezaje kuwaacha? Achilia mbali wazo zima la kuikata nchi yetu
Alexander Rodnyansky
Mshauri Mkuu wa Volodymyr Zelensky wa Ukraine
Alipendekeza toleo “halisi zaidi” la “mkataba wa Budapest” – ambalo liliipa Ukraine hakikisho la usalama – lingekuwa muhimu kufikia amani.
“Mkataba wa Budapest ulipaswa kuhakikisha usalama wetu kwa malipo ya kuacha silaha za nyuklia katika miaka ya 90.
“Inabidi iwe kitu kama hicho ambapo hatua zingebainishwa, ni nchi gani hasa zingechukua hatua kwa njia gani ikiwa usalama wako unatishiwa.”
Lakini alionya kwamba uwezekano wa kuhusika kwa nchi za Nato katika mapatano kama hayo itakuwa “suala tete”.
“Ndio maana mazungumzo sio rahisi, kwa sababu haungependa kuanzisha Kifungu cha 5, kimsingi, kuvuta Nato yote kwenye mzozo na Urusi.
“Hiyo ndiyo [ambayo] nchi za Nato hazitaki kutokea na ndiyo maana mazungumzo bado yanaendelea.”