Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani UNHCR, Filippo Grandi amesema watu milioni 10, ikiwa ni zaidi ya robo ya idadi jumla ya raia wa taifa hilo wamelikimbia kutokana kile alichokiita vita vya maangamizi vya Urusi.
Grandi amesema idadi hiyo inajumisha wakimbizi wa ndani au waliovuka mipaka ya taifa hilo tangu Urusi ianze uvamizi wake Februari 24. Asilimia 90 ya waliokimbia ni wanawake na watoto. Wanaume wa umri wa kati ya miaka 18 hadi 60 wanapsawa kuitika wito kusaidia jeshi na hawaruhusiwi kuondoka Ukraine.
Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima na watoto, UNICEF nalo limesema watoto milioni 1.5 ni miongoni mwa waliokimbilia uhamishoni, na kuonya hatari ya kukabiliwa na biashara haramu ya usafirishaji watu na utumikishwaji mbaya.
Kabla ya mgogoro huu wa sasa Ukraine ilikuwa na jumla ya watu milioni 37. Idadi hiyo inajumushia maeneo yaliokuwa katika udhibiti wa serikali ukiliondoa eneo lililonyakuliwa na Urusi la Crimea na maeneo ya wanaotaka kujitenga yenye kuunga mkono Urusi.