ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, May 30, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?

I am Krantz by I am Krantz
Mar 2, 2022
in HABARI
0
Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
0
SHARES
290
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

RUSSIA YAZIDISHA MASHAMBULIZI YA MAKOMBORA DHIDI YA UKRAINE

RUSSIA YAZIDISHA MASHAMBULIZI YA MAKOMBORA DHIDI YA UKRAINE

May 8, 2023
Load More


Rais Putin ameviweka vikosi vya nyuklia vya Urusi katika tahadhari “maalum”, na kuzua wasiwasi kote ulimwenguni.

Lakini wadadisi wa mambo wanadokeza kwamba hatua zake huenda zikatafsiriwa kuwa onyo kwa nchi nyingine kutozidisha ushiriki wao nchini Ukraine, badala ya kuashiria kutaka kutumia silaha za nyuklia.

Silaha za nyuklia zimekuwepo kwa takriban miaka 80 na nchi nyingi zinaziona kama kizuizi kinachoendelea kudhamini usalama wa taifa lao.

Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?

Takwimu zote za silaha za nyuklia ni makadirio lakini, kwa mujibu wa Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, Urusi ina vichwa vya nyuklia 5,977 – vifaa vinavyosababisha mlipuko wa nyuklia – ingawa hii inajumuisha takriban 1,500 ambazo zimechoka na zinatazamiwa kuvunjwa.

Kati ya 4,500 zilizosalia au zaidi, nyingi zinachukuliwa kuwa silaha za kimkakati za nyuklia – makombora ya balestiki, au makombora, ambayo yanaweza kulengwa kwa umbali mrefu. Hizi ndizo silaha ambazo kawaida huhusishwa na vita vya nyuklia.


Zilizosalia ni silaha ndogo za nyuklia zisizoweza kuharibu sana kwa matumizi ya masafa mafupi kwenye uwanja wa vita au baharini.

Lakini hii haimaanishi kuwa Urusi ina maelfu ya silaha za nyuklia za masafa marefu tayari kwenda.

Wataalamu wanakadiria takribani vichwa 1,500 vya kivita vya Urusi kwa sasa “vimetumwa”, kumaanisha kuwa viko kwenye kambi za makombora na mabomu au kwenye manowari baharini.

Je, hii inalinganishwaje na nchi nyingine?

Nchi tisa zina silaha za nyuklia: China, Ufaransa, India, Israel, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Marekani na Uingereza.


China, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza pia ni miongoni mwa mataifa 191 yaliyosaini Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Chini ya makubaliano hayo, wanapaswa kupunguza akiba yao ya silaha za nyuklia na, kwa nadharia, wamejitolea kutokomeza kabisa.

Na imepunguza idadi ya vichwa vya kivita vilivyohifadhiwa katika nchi hizo tangu miaka ya 1970 na 80.

India, Israel na Pakistan hazikuwahi kujiunga na NPT – na Korea Kaskazini iliondoka mwaka 2003.

Israel ni nchi pekee kati ya tisa ambayo haijawahi kukiri rasmi mpango wake wa nyuklia – lakini inakubaliwa na wengi kuwa na vichwa vya nyuklia.

Ukraine haina silaha za nyuklia na, licha ya shutuma za Rais Putin, hakuna ushahidi kuwa imejaribu kuzipata.

Silaha za nyuklia zina uharibifu gani?

Silaha za nyuklia zimeundwa kusababisha uharibifu mkubwa zaidi.

Kiwango cha uharibifu hutegemea mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

• Ukubwa wa kichwa cha silaha

• Jinsi inavyolipua juu ya ardhi

• Mazingira ya ndani

Lakini hata kichwa kidogo cha silaha ya kivita kinaweza kusababisha upotezaji mkubwa wa maisha na matokeo ya kudumu.

Bomu lililoua hadi watu 146,000 huko Hiroshima, Japan, wakati wa Vita vya pili vya dunia, lilikuwa kilotoni 15.

Na vichwa vya nyuklia leo vinaweza kuwa zaidi ya kilotoni 1,000.

Kidogo kinatarajiwa kuishi katika eneo la athari la mlipuko wa nyuklia.

Baada ya mwanga wa kupofusha, kuna moto mkubwa na wimbi la mlipuko ambalo linaweza kuharibu majengo na miundombinu kwa kilomita kadhaa.

Je, ‘kizuizi cha nyuklia’ kinamaanisha nini na kimefanya kazi?

Hoja ya kudumisha idadi kubwa ya silaha za nyuklia imetokana na uwezo wa kuwaangamiza kabisa adui yako ingewazuia kukushambulia.

Neno marufu zaidi kuelezea hili likawa uharibifu wa uhakika (Mad).

Ijapokuwa kumekuwa na majaribio mengi ya nyuklia na ongezeko la mara kwa mara la utata wa kiufundi na nguvu za uharibifu, silaha nza nyuklia hazitumiwi katika mapambano ya silaha tangu 1945.

Sera ya Urusi pia unazuia matumizi ya silaha za nyuklia na kuorodhesha hatu anne zinazoweza kuruhusu utumizi wa sillaha hizo:

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT

Related

Tags: MUSEVENIRUSSIA
ADVERTISEMENT
I am Krantz

I am Krantz

👉 FOUNDER & CEO of KONCEPT 👉Serial & Self-made Entrepreneur 👉Digital media consultant 👉Pr & media Guru/Awards winner Blogger 👉Startuper of the year 2016 by TOTAL 👉TOP 50 Most influential young Tanzania 2017 👉General Secretary at Tanzania Bloggers Network 👉 UPG Sustainability Leader in the Class of 2021 👉 ALUMNI The Tony Elumelu Foundation 👉Chairman YOUNG CEO CLUB Tanzania 🇹🇿 ‘ 😊 Marketer BY Education, Entrepreneur BY Profession & Blogger BY Passion ”😊

Related Posts

DIASPORA KUPEWA HADHI YA KIPEKEE
HABARI

DIASPORA KUPEWA HADHI YA KIPEKEE

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023
MAPACHA WALIOFARIKI ZIWANI WAKIOGELEA KUZIKWA MARA
HABARI

MAPACHA WALIOFARIKI ZIWANI WAKIOGELEA KUZIKWA MARA

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023
Legal Manager / Company Secretary Job Vacancy at BRAC Tanzania Finance LTD
HABARI

Legal Manager / Company Secretary Job Vacancy at BRAC Tanzania Finance LTD

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023
5 Various Job Vacancies at Tanzania Agricultural Development Bank (TADB)
HABARI

5 Various Job Vacancies at Tanzania Agricultural Development Bank (TADB)

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023
Digital Channels Manager Job Vacancy at Airtel Tanzania PLC
HABARI

Digital Channels Manager Job Vacancy at Airtel Tanzania PLC

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023
UMUHIMU WA KULA MATUNDA NA MBOGA MBOGA
HABARI

UMUHIMU WA KULA MATUNDA NA MBOGA MBOGA

by ALFRED MTEWELE
May 30, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
March 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031  
« Feb   Apr »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In